Na Hashim Aziz
Kilosa ni moja
kati ya wilaya zinazounda Mkoa wa Morogoro ikiwa na jumla ya wakazi 26,060 kwa
mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2002. Pia ni jimbo la uchaguzi
linaloongozwa na mwanasiasa mkongwe, Mustapha Mkulo kwa tiketi ya Chama cha
Mapinduzi (CCM).
Mkullo (kulia) |
MATATIZO YA WANANCHI
Katika ziara
hiyo, Uwazi lilibaini matatizo mbalimbali yanayowakabili wananchi wa jimbo hilo,
kubwa ikiwa ni mapigano ya mara kwa mara kati ya jamii za wakulima na wafugaji
wanaogombea ardhi kwa ajili ya kilimo na ufugaji, kama ilivyobainika pia katika
Jimbo la Mvomero ambalo pia lilitembelewa hivi karibuni.
Mkullo |
Wakulima wanalalamika kwamba wafugaji wa
Kimasai,
wamekuwa wakiingiza mifugo yao kwenye mashamba yao, jambo
linalosababisha hasara kubwa na kurudishwa nyuma kimaendeleo.
KERO
ZA WAKULIMA
“Kero yetu
kubwa sisi wakulima wa Kilosa ni wafugaji kuingiza mifugo yao kwenye mashamba
yetu na kuharibu mazao yetu hasa wakati wa kukaribia msimu wa mavuno. Tunaiomba
serikali kutuondolea kero hii ya miaka mingi.
“Unakuta
Wamasai wanamkabidhi mtoto mdogo wa miaka tisa au kumi kundi la ng’ombe zaidi
ya 100. Sasa unafikiri mtoto kama huyu atakuwa anajua thamani ya mazao ya
wakulima? Matokeo yake wanaingiza ng’ombe mashambani na kula mazao,” alisema Mzee
Joseph Jonas, mkazi wa Kibaoni anayejishughulisha na kilimo.
MATATIZO YA WAFUGAJI
Wafugaji nao
walikuwa na malalamiko yao wakidai kuonewa na wakulima na kupokonywa maeneo yao
ya kulishia mifugo.
“Sisi wafugaji
tunaoneka kama siyo raia wa nchi hii, kila tunapoingia kwenye pori tunafukuzwa
na kuambiwa tunaingiza mifugo yetu kwenye hifadhi, tukitafuta sehemu nyingine
tunaambiwa tunaingiza ng’ombe kwenye mashamba ya watu, sasa tukalishie wapi
mifugo yetu?
“Tunamuomba
mbunge atusaidie kwani wakulima wametukuta kwenye eneo hili, sisi tupo hapa
miaka mingi iliyopita sasa wanataka tuende wapi?” alisema Seliodi Ole Maleyo,
mfugaji wa Kimasai.
HUDUMA ZA KIJAMII
Mbali na tatizo hilo, wananchi
walieleza matatizo mengine yanayowasumbua kuwa ni uhaba wa maji safi na salama
ya kunywa, uhaba wa madarasa na vifaa vya kujifunzia, ukosefu wa madawa katika
hospitali na miundombinu mibovu, upungufu walimu na maabara kwenye shule za
sekondari na za msingi na kubwa zaidi, ukosefu wa huduma bora za kuwasaidia
wanawake wajawazito kujifungua salama.
“Kero yetu
kubwa sisi wanawake kwenye jimbo hili ni huduma duni kwenye hospitali yetu ya Wilaya
ya Kilosa. Kwa mfano mimi kama unavyoniona na mtoto wangu huyu mchanga, siku
zangu za kujifungua zilipokaribia, ilibidi nisafiri na tumbo langu hadi
Morogoro Mjini kwenda kujifungua.
“Huduma za
uzazi katika hospitali yetu ni za mashaka na usipokuwa makini unaweza kufa
hivyo tunamuomba mbunge wetu atusaidie
sisi wanawake,” alisema Rozina Seganje, mkazi wa Magomeni.
UKOSEFU WA AJIRA
Naye Kijana Athuman ldd Mkazi wa Uhindini
alisema: ”Kero yetu sisi vijana ni ukosefu wa ajira. Tunajua ajira hakuna
serikali hakuna lakini tunapotaka kujiajiri, tunakwamishwa na miundombinu
mibovu ya huku.
“Tangu awamu Rais
Mkapa, tuliambiwa kuwa kutajengwa barabra ya lami kutoka Dumila kupita kwenye jimbo
letu kueleka Mikumi hadi lringa lakini ni miaka kumi sasa imepita hakuna
kinachoendelea.
“Barabara
ikikamilika, tutafanya biashara na kujiajiri kwani kwa taarifa tulizonazo,
mabasi na malori yatakuwa yanapita hapa. Tunataka mbunge atuambie barabara hiyo
itakamilika lini au mpaka tufe?”
MAELEZO YA MBUNGE
Baada ya
kusikia kero hizo za wanananchi mwandishi wetu alipiga hodi nyumbani kwa Mbunge
Mkulo, Uhindini ambapo mlinzi wa nyumba hiyo alisema bosi wake yupo safarini
kikazi. Mwandishi wetu hakuchoka, akaamua kumwendea hewani ambapo
alipopatikana, alikuwa na haya ya kueleza:
“Ni kweli kero
hizo nazifahamu na kwamba naendelea kuzitafutia ufumbuzi ingawa baadhi ziko nje
ya uwezo wangu. Kwa sasa nipo Dodoma bungeni lakini kama upo kwenye jimbo langu,
baadhi ya kero kama hizo za hospitali na barabara nenda kwa DC (Mkuu wa Wilaya)
atakupa maelezo zaidi,” alisema Mkullo kwa kifupi kisha akakata simu.
No comments:
Post a Comment