Wengi wanamkumbuka kutokana na ukatili
wake kipindi alipokuwa madarakani na vita kali ya kugombea mpaka iliyopiganwa
kati ya nchi yake ya Uganda dhidi ya Tanzania, enzi hizo ikiwa chini ya Rais
Julius Kambarage Nyerere.
Anaitwa Idi Amini Dada, Rais wa tatu
wa Uganda aliyeingia madarakani baada ya kumpindua Rais Milton Obote na
yafuatayo ni mambo kumi usiyoyajua kuhusu dikteta huyu.
1. Katika kipindi alichokuwa
madarakani, kutoka 1971 hadi 1979, inakadiriwa kwamba aliwaua kikatili zaidi ya
watu laki tano waliokuwa wakienda kinyume na amri zake.
2. Aliwahi kuwa mwenyekiti wa OAU
(Organisation of African Unity) na alikuwa na ndoto za kuiunganisha Afrika kuwa
nchi moja ili aitawale, kama alivyokuwa akiwaza rafiki yake mkubwa, Muammar
Gaddafi.
3. Alikuwa na elimu ndogo aliyoipata
kwenye Shule ya Kiislamu ya Bombo na inaelezwa kuwa baadaye aliacha shule akiwa
hajui vizuri kuandika wala kusoma.
4. Mpaka anakufa, historia ya maisha
yake haikuwa ikifahamika vizuri. Wachambuzi wanaeleza kuwa alizaliwa Koboko
mwaka 1925, kutoka kabila la Kakwa.
5. Inaelezwa kuwa baada ya kuzaliwa, baba
yake mzazi, Andreas Nyabire alimtelekeza, akalelewa na mama yake mashambani, Kaskazini
Magharibi mwa Uganda mpaka alipokuwa mkubwa.
6. Baada ya kupinduliwa na majeshi ya
Tanzania mwaka 1978, alikimbilia Libya alikopewa hifadhi na Gaddafi na baadaye
kukimbilia Saudi Arabia alikofia kwa maradhi ya figo Agosti 16, 2003.
7. Alijiunga na jeshi la mkoloni, King's
African Rifles (KAR) mwaka 1946 akiwa mpishi msaidizi. Akawa anapanda vyeo
taratibu hadi alipofikia ngazi ya luteni mwaka 1961, akiwa mtu mweusi wa pili
kufikia cheo hicho. Akaendelea kupanda hadi alipojitangaza kuwa Field Marshal
kabla ya kupinduliwa.
8. Mbali na mambo ya jeshi na siasa,
Amini alikuwa mwanamichezo mashuhuri ambapo alikuwa akipigana masumbwi na pia alikuwa
muogeleaji.
9. Idi Amini alikuwa na wake zaidi ya
watano na jumla ya watoto 40. Mwaka 1974, aliwapa talaka wake zake watatu,
Malyamu, Nora na Kay kwa wakati mmoja na kuoa wengine.
10. Kulikuwa na tetesi za muda mrefu
kuwa Amini alikuwa akila nyama za watu na inadaiwa kuwa, mkewe mmoja ambaye
mpaka leo hafahamiki alipo, Nora aliuawa na kuliwa nyama na mumewe baada ya
kupewa talaka ingawa hakuna ushahidi wa kutosha.
No comments:
Post a Comment