Wengi huwa wanaamini unene ndiyo afya, kwamba mtu
mnene ana afya njema kuliko mwembamba lakini ukweli ni kwamba unene wa
kupindukia (obesity) ni tatizo ambalo kila anayependa kuishi maisha marefu
anapaswa kupigana nao.
Obesity ni hali ambayo mafuta yaliyozidi mwilini (excess
body fat) hujikusanya katika sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo kwenye moyo, na
kusababisha madhara makubwa ya kiafya kwa mhusika ikiwemo magonjwa ya moyo,
kisukari au wakati mwingine vifo vya ghafla.
UTAJUAJE
KAMA UNA OBESITY?
Wengi hushindwa kuelewa kama unene walionao ni wa
kawaida au la, naamini baada ya kusoma mada hii, kila mmoja atakuwa na uwezo wa
kujitambua mwenyewe bila hata kwenda kwa daktari.
BODY
MASS INDEX (BMI)