Msechu |
Alpha, mshiriki wa Rwanda katika shindano la Tusker Project Fame linalofanyika Kenya kwa kushirikisha nchi za Afrika Mashariki, amesema kuwa anafurahi kushindana na Mtanzania Peter Msechu kwa sababu ana kipaji cha hali ya juu.
Project Fame katika season hii imepewa jina la All Stars kwa maana inashirikisha washindi na washiriki wengine waliowahi kutamba katika mashindano yaliyotangulia.
Akijibu swali la MC wa shindano hilo, Gaetano Kagwa kuhusu namna anavyojisikia kurudi kwenye mpambano huo mwaka huu, Alpha ambaye ni mshindi wa mwaka 2009 alisema: “Nafurahi sana. Ni bahati sana kupewa nafasi nyingine ya kushindana.
“Si kweli kuwa nimekuja nikiwa na imani kwamba lazima nitashinda, ila hili ni shindano, hakuna mtu anayeweza kuwa na dhamira ya kushindwa. Nitashindana ili nishinde.
“Changamoto ni kubwa, unajua kuingia kwenye shindano na msanii mwenye kipaji kikubwa kama Msechu inabidi ujipange. Namkubali sana Msechu ni mkali.”
Alpha alisema, mwaka jana alifuatilia kwa ukaribu shindano hilo na alivutiwa na uwezo mkubwa uliooneshwa na Msechu.
Mwaka huu, Tanzania imeingiza washiriki wawili, Mseche na Hemed Suleiman.
No comments:
Post a Comment