Sunday, April 24, 2011

My Heart inaendelea

Inaendelea... Alipofika uani, alishtukia taa zote zikizimwa, akajitupa chini na kubiringika mpaka chini ya kibanda cha kuku kilichokuwa pale uani, akatulia kimya akisubiri kitakachotokea. Akasikia vishindo vya mtu akija kule alikojificha. Wakati hayo yakiendelea, alisikia mwalimu Kihiyo akilalamika kwa maumivu kutoka chumbani kwake, kisha ukasikika mlio wa risasi mfululizo uliofuatiwa na yowe kuu la mwalimu Kihiyo, akajua kwa vyovyote amepigwa risasi.
Alichohisi kilikuwa kweli. Yale majambazi yalikivamia chumba anacholala mwalimu. Kihiyo na mkewe, yakawa yanamshinikiza aeleze ni wapi alikowaficha Mzee Khalfan na familia yake. Alikataa kufanya hivyo na badala yake akakimbilia mahali alikoficha bastola yake lakini kabla hakafanya lolote alishtukia mvua ya risasi ikimnyeshea mwili mzima... Akadondoka na kupiga yowe kuu, akajinyoosha na kutulia tuli. Baada ya kushuhudia mumewe akiuawa kikatili, Mke wa mwalimu Kihiyo alianza kupiga kelele kama mwendawazimu. Yale majambazi yakamuamrisha kueleza walikowaficha Khalfan na familia yake. Kwa jinsi yalivyokuwa hayana masihara, aliona na yeye angeuawa...

No comments:

Post a Comment

THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 1

Mtunzi: Hashim Aziz (Hashpower) 0719401968 “Ngo! Ngo! Ngo! Fungua!” “Nanii?” “Fungua!” “Jitambulishe kwanza, wewe nani?” “Nimese...