PART II OF SHED NO MORE TEARS GENEVIV
Baada ya majeraha kupona, huacha makovu ikiwa ni alama ya maumivu yaliyopoa na kuisha. Maisha alyopitia Geneviv, yaliyojaa misukosuko na matatizo ya kila aina, hatimaye yanafikia ukingoni na Geneviv anaanza ukurasa mpya wa maisha yake. Majeraha makubwa aliyojeruhiwa mtimani na akilini mwake yanapona na kuacha makovu makubwa, makovu ambayo nayo yanafutika taratibu. Anasahau kila kitu na kwa msaada wa mama yake mpendwa anafanikiwa kurudi tena shuleni.
Lile tabasamu lilipotea kwa muda mrefu linaanza kuchanua upya usoni mwake na kuufanya uzuri wake wa asili uliopotea kwa muda mrefu kuanza kuchanua mithili ya jua la asubuhi. Ndoto zote ambazo zilikuwa zimepotea na kufutika maishani mwake mithili ya theluji juani sasa zilianza kurudi upya.
Uzuri wa sura na umbo lake vinajidhihirisha upya na kumfanya kila anayemuona kumshangaa na kumsifia kuwa amebarikiwa.
Huwezi kuamini kuwa huyu ndiye Geneviv aliyekuwa akilia na kuomboleza karibu kila siku maishani mwake kutokana na shida za dunia hii. Kila kitu kinabakia kuwa Historia na anamwachia Mungu kwani ni kwa kudra zake ndizo zilizomuwezesha kuwa hai mpaka muda huo.
********
Maisha mapya akiwa kama mwanafunzi wa sekondari, yalimfurahisha sana na akajikuta akijilaumu kwa nini alichelewa kuanza shule. Marafiki zake aliosoma nao shule ya msingi walikuwa mbele kwa kidato kimoja kutokana na yeye kupoteza mwaka mzima nyumbani kutokana na matatizo yaliyokuwa yanaiandama familia yao.
Hilo lilimtia uchungu kiasi, lakini moyoni alijiapiza kuwa ataendelea kuwa bora kuliko hata hao waliomtangulia. Baada ya muda mfupi tu tangu aandikishwe kuanza sekondari, Geneviv alishaanza kufahamika shule nzima, akijizolea marafiki wapya lukuki.
Alianza kung’ara darasani akionyesha uwezo mkubwa sana kwenye masomo, hasa elimu ya Viumbe hai (Biology), Hesabu na masomo mengine ya sayansi. Walimu wake walianza kumtabiria kuwa atakuja kuwa daktari Bingwa baadae kutokana na kuyamudu vizuri masomo ya Sayansi.
“Mama eti mwalimu kaniambia mi nafaa kuwa Daktari, Aka mi staki! Nataka kuwa mwanasheria kama baba’ake Kim ili niwatetee watoto na wanawake wanaodhulumiwa haki zao”, Aliongea Geneviv akimueleza mama yake, muda mfupi baada ya kutoka shule.
Mama yake alitabasamu na kumwambia akaze buti zaidi kwenye masomo na asijihusishe na mambo mengine kwani madhara yake alikuwa akiyafahamu vizuri. “lakini tangu unaanza darasa la kwanza ulisema unataka kuwa Daktari, Mbona leo unabadilisha maamuzi yako mwenyewe?”
Bi Patricia alimuuliza mwanae na wakawa wanapiga stori kirafiki. Geneviv alimueleza kuwa anatamani kuwa mwanasheria baada ya kugundua kuwa kuna wanawake na watoto wengi ambao wanakosa haki zao, wananyanyasika kijinsia na kuonewa kwa sababu hakuna mtu wa kuwasaidia.
Siku hizi naona umekua maana hata upeo wako wa kufikiri nao umeongezeka na unaongea mambo ya kiutu uzima zaidi, Bi Patricia alimsifia mwanae na wote wakatabasamu kwa furaha.
Maisha kwao yalikuwa ni kama yameanza upya kabisa, wakiongea na kufurahi kama zamani. Pengo kubwa lililokuwa limebakia lilikuwa ni kufiwa na baba wa familia, Bwana Rwakatare. Bi Patricia alijitahidi kwa kadri ya uwezo wake wote kuliziba pengo lile na kumfanya Geneviv asilione pengo lililokuwepo, alifanikiwa kwani Geneviv hakuona tofauti yoyote.
Kwa kawaida baada ya muda wa masomo, Geneviv na mama yake walikuwa wakienda kujumuika na watoto waliokuwa wanaishi katika mazingira magumu na mayatima, ambao kwa msaada wa Bwana Magwaza walifanikiwa kuwafungulia kituo maalum. Geneviv alikuwa akipenda kuwafundisha nyimbo za kiingereza alizofundishwa shuleni kwao.
Watoto wote walitokea kumpenda, kiasi kwamba asipoonekana hata siku moja walikuwa wakimuulizia sana mama yake, ambaye ndiye aliyekuwa mlezi mkuu wa kituo kile. Maisha yakawa yameongezeka msisimko kuliko awali. Siku zikawa zinasonga na maisha yakawa yanasogea mbele, Geneviv akizidi kukua na kupendeza zaidi.
Shuleni kwao, taratibu wanafunzi wa kiume walianza kujigonga kwa Geneviv kila mmoja akitaka awe rafiki yake. Kutokana na kumbukumbu mbaya zilizokuwa zimeanza kufutika akilini mwake juu ya ukatili aliowahi kufanyiwa na wanaume zilizimfanya awachukie wavulana kupita kawaida.
Alishajiwekea nadhiri akilini mwake kuwa kama haitawezekana kwa yeye na Kim kuja kuwa baba na mama, basi ni bora kuishi peke yake maishani mpaka atakapozeeka na kufa. Japokuwa walikuwa wametenganishwa kabisa na Kim, daima aliendelea kuwa moyoni mwake na alishamsamehe kuhusu kila kitu kilichotokea, na zaidi alimuona kama shujaa maishani mwake.
“He is my Hero! I will never Forget him” (Yeye ni Shujaa wangu! Sitamsahau maishani mwangu)
Geneviv alikuwa akiongea peke yake jioni moja akiwa amejifungia chumbani kwake akizitazama picha alizokuwa amepewa na Kim kabla hawajatenganishwa.
Kilichomfanya mpaka ashindwe kumsahau Kim ni upendo wa dhati aliomuonesha kipindi wakati wakiwa na matatizo yaliyowafanya wapteze matumaini ya kuishi, yeye na mama yake. Alikuwa akikumbuka mambo mengi ambayo Kim alimfanyia, ambayo haikuwa kawaida kwa binadamu wa kawaida kuyafanya. Alizidi kuamini kuwa Kim alikuwa ni zawadi ya kipekee kwake aliyoshushiwa kutoka mbinguni.
Kumbukumbu za matukio ya mwisho yaliyotokea na kupelekea Geneviv kutaka kujitoa roho, zilimfanya ajione kama aliyeshindwa kulpa fadhila kwa mema yote aliyotendewa na Kim. Alijikuta akimchukia sana Alice kwani aliamini yeye ndiye aliyekuwa chanzo cha yote, lakini kwa kuwa alikuwa ameamua kuanza ukurasa mpya wa maisha yake, alimsamehe kutoka moyoni mwake na akaendelea kuamini kuwa ipo siku Mungu atawakutanisha tena.
“Mama mi shuleni nasumbuliwa sana na wavulana. Everyone is seducing me! Im Bored and I don’t like them…they are devils” ( Kila mmoja ananitongoza mpaka naboreka! Siwapendi kabisa… wavulana ni mashetani), Geneviv alikuwa akimsimulia mama yake wakati wakiandaa chakula cha jioni. Ilibidi Bi Patricia acheke baada ya mwanae kumweleza.
“You are very Beatiful my Daughter, hata kama ningekuwa mimi ndio mvulana halafu nasoma darasa moja na wewe lazima ningekutaka tu”, Aliongea kwa masihara Bi Patricia na wakaishia kucheka kwa furaha. Alimtoa wasiwasi kuwa asiogope kutongozwa kwani hiyo ilikuwa ni kama sifa tosha kwa binti mrembo kama yeye, ila akamsihi kuwa asikubali kujiingiza kwenye uhusiano wa kimapenzi na mtu yeyote kwani hata yeye alishaona madhara yake.
“Jitulize na kazania masomo mwanangu, utampata tu atakayekufaa maishani”, Bi Patricia alizidi kumuasa mwanae. Geneviv aliitikia kwa kutingisha kichwa huku akili yake yote ikimuwaza Kim. Alijiapiza kuwa hatarudia makosa kama ya awali na akajiapiza kuwa atajitunza kwa kadri ya uwezo wake wote, ilimradi ndoto yake itimie, ya kuja kuolewa na Kim.
********
Kim alikuwa naye ameyaanza maisha mapya, akiwa mabli kabisa na kwao. Mazingira ya jii la Nairobi yalikuwa tofauti na mazingira ya nyumbani kwao, Blazinia. Shule ya sekondari ya wavulana ya Kasarani Boys Camp Nairobi aliyokuwa anasoma, ilikuwa tofauti kabisa na St Benedict Seminary aliyokuwa anasoma awali.
Japokuwa shule ilikuwa na mandhari ya kisasa, alipata shida kubwa kuzoeana na wanafunzi wenzake. Hali ya hewa nayo ilikuwa ni tatizo jingine kwake kwani alikuwa akisumbuliwa sana na tatizo la kifua kubana.
Miezi miwili aliyokaa shuleni hapo ilikuwa ni kama mwaka mzima. Licha ya kusumbuliwa na mazingira na hali ya hewa, bado akili yake ilikuwa ikimuwaza sana Geneviv. Kilichofanya amuwaze namna ile ni hisia za kushtakiwa na dhamira zilizokuwa zikitawala maisha yake. Hakuhesabu mazuri aliyowahi kumfanyia Geneviv, alichokikumbuka ilikuwa ni maumivu aliyomsababishia Geneviv mpaka akafikia hatua ya kutaka kujiua.
Alikuwa akijisikia vibaya sana kila alipokumbuka tukio lile. Alitamani kupata muda wa kumuomba msamaha Geneviv ili abakie na amani moyoni mwake, lakini hilo halikuwezekana. Umbali ulikuwa ni kigezo kikubwa kilichofanya isiwezekane.
Aliamini kuwa isingekuwa rahisi kwa geneviv kukubali kuendeleza uhusiano wao uliovunjika katika hatua za mwanzo kutokana na tukio lile, lakini alichokitaka ilikwa ni kusikia kauli ya Geneviv akimwambia kuwa amemsamehe.
Hakutaka kuendelea kumuwaza sana Geneviv kwani alijua fika kuwa ni mawazo hayohayo ndiyo yaliyomfanya akijikuta anaangukia katika tatizo kubwa la matumizi ya madawa ya kulevya. Hakutaka jambo lile lijirudie tena. Akaona njia bora ni kumsahau jumla na kumtoa kabisa mawazoni mwake. Aliamini kuwa kama Mungu wake amemsamehe basi kila kitu kilikuwa kimekwisha.
Aliamua kwa moyo mmoja kuelekeza nguvu zake zote kwenye masomo na kuzoea mazingira mapya. Licha ya kujitahidi kwa kadri ya uwezo wake wote, bado hisia za ndani ziliendelea kumshtaki. Ukweli wa kuwa alikuwa amempenda Geneviv kuliko kitu chochote maishani mwake uliendelea kumtesa moyoni mwake.
Stay Tunned!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 1
Mtunzi: Hashim Aziz (Hashpower) 0719401968 “Ngo! Ngo! Ngo! Fungua!” “Nanii?” “Fungua!” “Jitambulishe kwanza, wewe nani?” “Nimese...
-
Ni wiki nyingine ambapo mwenyezi Mungu ametujaalia kukutana katika busati letu la mahaba ambapo tunajadiliana mambo mbalimbali yanayohusu ...
-
HASH POWER 7113 NI matumaini yangu kwamba msomaji wangu uko poa. Ni wiki nyngine tunapokutana kwenye busati letu ambapo tunajuzana na kuja...
No comments:
Post a Comment