ILIPOISHIA:
Muda mfupi baadaye, wote tulikuwa
‘saresare maua’, akanisukuma kwa nguvu kwenye uwanja wa fundi seremala,
nikaangukia mgongo, akaja juu yangu kwa kasi, maandalizi ya mechi ya kirafiki
isiyo na jezi wala refa yakaendelea huku akionesha kunikamia kama Simba na
Yanga zinavyokamiana zinapokutana uwanjani.
SASA ENDELEA...
Kipyenga kilipolia tu, Shamila ndiye
aliyekuwa wa kwanza kugusa mpira, akawa anabutua mashuti ya nguvu na kunifanya
nihisi kama atanielemea na kunishinda ndani ya muda mfupi tu, jambo ambalo
kwangu lingekuwa aibu kubwa.
Nikajipanga na kuanza kwenda naye sawa,
akawa akipiga mashuti kwa kubutua, mimi naukontroo mpira na kumpiga chenga za
mwili, wakati mwingine nikawa natambaa na chaki kama Christiano Ronaldo, jambo
lililofanya kibao kigeuke, badala ya yeye kuwa ananishambulia kwa kasi, ikawa
mimi ndiyo namshambulia.
Ilibidi nitumie ujuzi wa hali ya juu
kuwahi kummaliza nguvu ili nimalize mchezo kwani Junaitha naye alikuwa
akinisubiri na sikujua alikuwa na lengo gani. Kutokana na jinsi nilivyokuwa
namshambulia Shamila kwa akili, haikuchukua muda mrefu, akatangaza kusalimu
amri, akanikumbatia kwa nguvu!