HASH POWER 7113
ILIPOISHIA:
Mabishano makali yaliendelea kwa muda, ikabidi yule mganga ajibadilishe sura na kuanza kuonekana kama bibi yake Gamutu, Bi Lubunga kisha akajitokeza mbele yake ili aamini.
“Haa kumbe ni wewe bibi?” Alihoji Gamutu huku akimuachia Fatiha na kuanza kuelekea kule yule mganga alikokuwa amesimama. Akachomoa kichupa kilichokuwa na unga mweusi, akaupuliza angani, Gamutu akaanza kujihisi kulegea viungo vvote vya mwili wake.Akahisi kizunguzungu kikali, akamuona yule mganga akimsogelea na kubadilika sura tena, akamshika mikono kisha akazungumza maneno kadhaa ambayo hakuyaelewa, wakapotea kimiujiza.
Kituo cha kwanza kilikuwa ni makaburini, mahali walipokuwa wanafanyia tambiko la kumkomboa Gamutu. Yule mganga alipomfikisha Gamutu akiwa hajitambui, kila mmoja alipiga vigelegele kwa furaha kwani hatimaye kazi ile nzito ilikuwa imekamilika. Wakaendelea na tambiko usiku kucha, Gamutu akiwa amepoteza fahamu. Kulipopambazuka, wakambeba na kuanza kumrudisha nyumbani kwa Bi Lubunga.
SASA ENDELEA…
Mganga wa kwanza alitangulia mbele akiwa na chungu kilichokuwa kinawaka moto ndani yake, yule wa pili akawa ameshika kitanda cha kamba pamoja na Bi Lubunga ambacho walikuwa wamemlaza Gamutu aliyekuwa amepoteza fahamu. Kwa pamoja walikuwa wakiimba mapambio ambayo haikueleweka yalikuwa ni dini gani, huku yule wa mbele akimwaga vitu kama dawa njia yote waliyokuwa wanapita.
Waganga hawa wanawake ndiyo waliyomfanyia Gamutu tambiko la kwanza la maisha. Nguvu zao zilikuwa zikiaminika Sumbawanga yote, na hata miujiza waliyokuwa wanaifanya ilisababisha wengine kuwaita ‘mapacha wa moto’. Hii ndiyo sababu iliyofanya Bi Lubunga aende kuomba msaada moja kwa moja kwao kwani ndiyo pekee waliokuwa wanamuelewa vizuri pamoja na nguvu alizozaliwa nazo.
Mapambazuko yaliwapokea vizuri kwani kwa kadri walivyozidi kusogea nyumbani kwa Bi Lubunga ndivyo kulivyozidi kupambazuka. Kazi nzito waliyoifanya makaburini kwa siku mbili mfululizo ilikuwa imezaa matunda na sasa kila mmoja alikuwa akimshukuru Mungu wake kwa yaliyotokea.
“Gamutu! Gamutu! Amka mjukuu wangu…,” Bi Lubunga alikuwa akimuita mjukuu wake wakati wale waganga wamemlaza kwenye kitanda cha kamba chumbani kwake huku chini wakiwa wameweka karai lenya maji yaliyochanganywa na dawa za kienyeji, ambayo mvuke wake ulikuwa ukimpitia Gamutu.
Mpaka inatimu saa moja asubuhi, Gamutu alikuwa bado hajazinduka. Wale waganga walikuwa wakizidi ‘kufanya mambo’ huku wakitumia ujuzi wao wote kuhakikisha muunganiko wa nguvu za Gamutu na majini unavunjika. Hakuna aliyekuwa na jibu la moja kwa moja kwamba kwa nini Gamutu amevutwa kirahisi namna ile na nguvu za kijini.
s Haikuwa kawaida kwa binadamu kwenda kuhisi kwenye himaya ya majini kisha kurejea. Binadamu siku zote huishi duniani na majini ujinini, kwa Gamutu ilikuwa ni zaidi ya maajabu. Ilipotimu saa tatu asubuhi, Gamutu alifumbua macho na kwa mara ya kwanza akazungumza.
“Bibi yangu yuko wapi?”
“Nipo Gamutu, nipo mjukuu wangu, pole!”
“Kwani bibi unanipa pole mimi nimefanyaje?
“Hapana Gamutu, hamna kitu, nakupa pole kwa safari ndefu,” aliongea Bi Lubunga huku akimsogelea pale kitandani na kutaka kumkumbatia… wale waganga wakamzuia na kumweleza kuwa kwa kufanya vile na yeye ataambukizwa nguvu za kijini kwani zilikuwa bado hazijaisha mwilini mwake.
Alisikia maelekezo aliyopewa, akarudi nyuma, dawa ikazidi kuchochewa na sasa mvuke mwingi ukawa unamlowanisha Gamutu na kumfanya apige chafya nyingi. Wale waganga waliendelea kufanya mambo yao, hawakuchoka na hawakuwa na dalili hiyo. Bi Lubunga aliwashangaa kwani kwa siku mbili mfululizo hawakupata hata muda wa kupumzika.
Akajua kweli walikuwa na lengo la kweli la kuhakikisha mjukuu wake anakombolewa. Kwa moyo mkunjufu akaongeza malipo ya ng’ombe na kondoo mwingine mweupe kama nyongeza ya makubaliano ya awali.
Mpaka inatimia saa kumi na moja jioni, Gamutu alikuwa tayari amerejewa na fahamu zake timamu, akawa na uwezo wa kuwatambua watu na kuzungumza lugha inayoeleweka. Hata hivyo, wale waganga hawakuondoka. Walitaka kuhakikisha nini kitatokea usiku wa manane. Kama siku hiyo ingepita bila chochote kutokea, hiyo ingemaanisha kuwa tayari Gamutu yuko huru. Hakuna ambaye alikuwa na uhakika wa nini ambacho kitatokea, lakini kwa kuwa wote walikuwa na imani kali juu ya mizimu na nguvu za giza, waliamini watavishinda vikwazo vyote.
***
Fatiha aliendelea kulala akiwa hajitambui pale alipochukuliwa Gamutu. Nguvu zilikuwa zimemwisha kabisa kwani wale waganga walimvizia akiwa ametoka kusababisha ajali duniani ambazo zilimlazimu kutumia nguvu zake zote za kijini, akabaki mwepesi. Wakamvamia na kumzidi kete kwenye ulimwengu wa giza. Hiyo ndiyo ilikuwa sababu ya kumwokoa Gamutu kirahisi, vinginevyo wasingeweza.
Usiku mzimaulipita bila Fatiha kurejewa na fahamu. Hata wenzako walipoamka kwa ajili yasala yaalfajiri, yeye alikuwa bado hajarudi kwenye hali yake ya kawaida. Mapambazuko yalikmkuta akiwa bado hajitambui.
“Kuna mmoja wenu hajaonekana tangu alfajiri, yu wapi malkia wa uvumilivu Fatiha? Ewe mkuu! Fatiha alionekana bustanini na ‘kiti mgeni’, wakicheza michezo ya kimahaba, kisha harufu ya damu ikafuatia, sote tuliisikia… ilikuwa inafanana na ya malkia wa uvumilivu Fatiha.”
Maelezo yale yalifanyiwa kazi ndani ya sekunde chache, bustani nzima ilizingirwa na Fatiha akaonekana kando ya waridi akiwa amelala huku damu nyingi zikiwa zimeganda pembeni yake na kutengeneza mfan wa bwawa ladamu.
“nini kimempata?”
“Atakuwa ameponzwa na mapenzi!”
“Hapana, amefanya kazi kubwa kuliko ninyi nyote usiku uliopita akiwa sambamba na ‘kiti mpya’. Atakuwa amekumbana na nguvu mbaya duniani, mpelekeni joshoni haraka akaoge na kutoa nuksi. Fanyeni haraka,” sauti yenye mamlaka ilisikika, kundi kubwa likajipanga kufanya kazi ile.
Ilipangwa kuwa akizinduka tu, aeleze nguvu mbaya kutoka duniani zimempataje, kisha kisasi kingetekelezwa haraka kabla ya usiku wa manane haujaisha. Akiwa kwenye usingizi ule wa kifo, Fatiha alijishangaa akiweza kuuvaa ubinadamu wa kawaida kama Gamutu na kukaa pembeni yake, ingawa kwa kutumia sura ya kijini ambayo inaweza kubadilika na kuwa binadamu endapo mhusika ataamua. Alisimama kando ya kitanda cha kamba alichokuwa amelazwa Gamutu akifanyiwa tiba na waganga wa kienyeji. Kwa kuwa ngtuvu zake za kijini zilikuwa zimenyonywa na mabaki yake kubakizwa ndani ya bustani ulipokuwa mwili wake wa kijini, hakuwa na nguvu duniani zaidi ya kubakia mtazamaji.
Akawa anaangalia kilakaitu anachofanyiwa Gamutu. Moyoni alijua kuwa kama ahatarejewa na nguvu zake za kijin haraka kabgla wale waganga hawajamalizia tambiko lao, asingeweza kumpata tena kipenzi cha moyo wake. Machozi yakawa yanamtoka huku akisubiri huruma ya majini wenzake kuutafuta wili wake kasha kuuongezea ngtivu kama wafanayavyo majini siku zote.
No comments:
Post a Comment