Acreditation: Global Publishers
KIFO cha msanii wa Hip Hop Bongo, Albert Kenneth Mangwea a.k.a Ngwea kilichotokea Jumanne wiki hii jijini Johannesburg, Afrika Kusini ‘Sauzi’, kinaendelea kuibua mapya ambapo sasa sumu imetajwa kuhusika, Hashpower7113 linafungua kila kitu.
Hospitali aliyopelekwa
Akizungumza na paparazi wetu juzi kwa njia
ya simu moja kwa moja kutokea nchini humo, Mtanzania mmoja (jina tunalo)
alisema muda huo yeye alikuwa nje ya Hospitali ya St. Helen Joseph
ambako mwili wa marehemu ulikuwa umehifadhiwa kwenye Mochwari ya
Hillbrow.