HASH POWER 7113
Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa alipokuwa anamnadi Kafumu kwenye kampeni |
Aliyekuwa mbunge wa Igunga, Tabora kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dalali Peter Kafumu amevuliwa ubunge wa jimbo hilo na Mahakama Kuu Kanda ya Tabora baada ya kubainika kuwa hakumshinda kihalali mpinzani wake, Kashinje wa Chadema.
Mahakama hiyo imechukua hiyo leo baada ya kuridhishwa na ushahidi wa pande zote mbili ambapo pia imebainika kuwa viongozi mbalimbali wa kiserikali, wakiwemo mawaziri na viongozi wastaafu walishirikiana kuwarubuni na kudaiwa kutoa rushwa kwa wananchi wa jimbo hilo ili Kafumu ashinde.
Habari hizo si nzuri kwa wanachama wa CCM ingawa kwa upande mwingine zimepokelewa kwa shangwe na mashabiki wa vyama pinzani hususan Chadema.