SEVEN DAYS IN HELL (SIKU SABA KUZIMU)- 63ILIPOISHIA:
Muda mfupi baadaye, wote tulikuwa ‘saresare maua’, akanisukuma kwa nguvu kwenye uwanja wa fundi seremala, nikaangukia mgongo, akaja juu yangu kwa kasi, maandalizi ya mechi ya kirafiki isiyo na jezi wala refa yakaendelea huku akionesha kunikamia kama Simba na Yanga zinavyokamiana zinapokutana uwanjani.
SASA ENDELEA...
Kipyenga kilipolia tu, Shamila ndiye aliyekuwa wa kwanza kugusa mpira, akawa anabutua mashuti ya nguvu na kunifanya nihisi kama atanielemea na kunishinda ndani ya muda mfupi tu, jambo ambalo kwangu lingekuwa aibu kubwa.
Nikajipanga na kuanza kwenda naye sawa, akawa akipiga mashuti kwa kubutua, mimi naukontroo mpira na kumpiga chenga za mwili, wakati mwingine nikawa natambaa na chaki kama Christiano Ronaldo, jambo lililofanya kibao kigeuke, badala ya yeye kuwa ananishambulia kwa kasi, ikawa mimi ndiyo namshambulia.
Ilibidi nitumie ujuzi wa hali ya juu kuwahi kummaliza nguvu ili nimalize mchezo kwani Junaitha naye alikuwa akinisubiri na sikujua alikuwa na lengo gani. Kutokana na jinsi nilivyokuwa namshambulia Shamila kwa akili, haikuchukua muda mrefu, akatangaza kusalimu amri, akanikumbatia kwa nguvu!

“Nakupenda sana Jamal, nataka unioe, nataka niwe mkeo wa ndoa,” alisema Shamila kwa sauti kama mtoto mchanga, nikamnong’oneza sikioni kwamba asiwe na wasiwasi, nitamuoa, nikamuona akitabasamu na kuangukia upande wa pili kama mzigo. Haikuchukua muda, akawa anakoroma kuonesha kwamba tayari alishapitiwa na usingizi mzito, hakujua kama nilikuwa nacheza na akili yake.
Kwangu mimi ilikuwa ni zaidi ya ushindi kwani nilijua sasa hatanisumbua tena. Harakaharaka nikainuka na kuchukua gwanda zangu na kuzitia mwilini, ikabidi nirudi kwanza kwenye chumba changu. Harakaharaka nikaenda kujimwagia maji huku nikitafakari kilichotokea muda mfupi uliopita.
Kiufupi nilikuwa nimebadilika sana, sikuwa Jamal yule ambaye hata mimi mwenyewe najijua. Awali nilikuwa muoga sana wa wanawake, hata Raya, msichana aliyetokea kunipenda kwa moyo wake wote, ilinichukua muda mrefu sana mpaka kuja kukutana naye kimwili lakini sasa, nilikuwa kama jogoo, kila tetea anayepita mbele yangu sikuwa naona hatari kumpitia. Hata sielewi ujasiri huo niliupata wapi.
Wakati nikiwa naendelea kujimwagia maji, ni kama Junaitha alichoka kunisubiri kule chumbani kwake, nikashtukia akiingia chumbani kwangu. Nilimtambua kuwa ni yeye hata kabla sijamuona kutokana na jinsi alivyoniita.
“Mbona huji jamani, mi nakusubiri mpaka nachoka bwana!” alisema huku akikaa kitandani. Nikamwambia kuwa nilikuwa nasikia sana joto kwa hiyo niliamua kujimwagia maji kabisa.
“Sasa si ungekuja kulekule kwangu uoge?” alisema. Kwa kuwa tayari nilishamaliza, nilijifunga taulo na kutoka.
“Utasababisha hawa watoto wajue siri yetu bure! Nataka nikiingia chumbani na wewe uwe umeshafika,” alisema kwa sauti yenye mamlaka, nikacheka huku nikijifuta maji. Alisimama na kusogea mlangoni, akachungulia huku na kule, alipoona hakuna mtu, alitoka na kuusindika mlango.
Harakaharaka nilivaa nguo zangu, nikatoka na kufunga mlango, nikatembea kwa umakini mpaka kwenye mlango wa chumba cha Junaitha, nikausukuma, ulikuwa wazi, nikaingia mpaka ndani.
Wewe ni mwanaume wa kipekee sana Jamal, samahani usione kama nakufosi kuwa na mimi kwa sababu nimekuzidi kila kitu na hapa upo kwangu, hapana! Ni kwa sababu sijawahi kukutana na mwanaume kama wewe maishani mwangu. Mtu anaweza kukuona mdogo kwa nje lakini una mambo makubwa sana,” alisema Junaitha na kunisogelea, akanikumbatia kwa nguvu, nikalihisi joto la mwili wake kwenye mwili wangu.
Japokuwa nilikuwa nimetoka kwenye mchezo muda mfupi uliopita, kwa jinsi Junaitha alivyokuwa akihamasisha, nilijikuta nikiwa tayari kwa mpambano mwingine, japokuwa hata sheria za mchezo hazikuwa zikiruhusu kilichokuwa kinataka kufanyika.
Haukupita muda mrefu, tuliingia uwanjani tena lakini tofauti na Shamila, Junaitha alikuwa na utaalamu wa hali ya juu. Naye hakuwa na papara kama mimi, maandalizi ya kupasha viungo moto yalienda taratibu, kipyenga kilipopulizwa, kila mmoja akawa anacheza kwa staili ya kumvizia mwenzake, ladha ya mchezo ikawa tofauti kabisa na Shamila.
Mtanange wa kukata na shoka uliendelea, hata sijui nguvu za kuhimili mikikimikiki nilizipata wapi kwa sababu kwa jinsi nilivyomudu kucheza na mpira, hata Junaitha mwenyewe hakugundua kwamba nimetoka kulisakata tena kabumbu muda mfupi tu uliopita.
Mpaka kipyenga cha mwisho kinapulizwa kuashiria kumalizika kwa mpambano huo, Junaitha alikuwa hajitambui, nikajikokota na mpira wangu kwapani kwa sababu kama sheria zinavyosema, mchezaji akipiga hat trick anaondoka na mpira wake, nikavaa gwanda zangu na kurudi chumbani kwangu, nikimuacha Junaitha naye anakoroma.
Nilipofika na kujitupa kitandani, kutokana na jinsi nilivyokuwa nimechoka, sikuelewa tena kilichoendelea mpaka nilipokuja kuzinduka alfajiri ya siku ya pili. Junaitha ndiye aliyekuja kuniamsha, cha ajabu eti akawa ananilaumu kwamba kwa nini sikulala kule kwake, akawa ananiuliza niliondoka muda gani? Nikajua kwamba kwa vyovyote na yeye ndiyo alikuwa amezinduka alfajiri hiyo.
Kwa kuwa siku hiyo tulikuwa na ratiba ngumu sana, tulianza kujiandaa, tukawaamsha watu wengine wote ambapo Shamila alikuwa mgumu sana kuamka kwa madai kwamba bado mwili wake ulikuwa umechoka, ikabidi Junaitha atumie nguvu.
Saa kumi na mbili juu ya alama, wote tayari tulikuwa tumeshajiandaa, tukakaa mezani na kunywa chai iliyoandaliwa na Junaitha kisha baada ya hapo, tukatoka. Ilibidi tutumie gari la Junaitha ambalo kabla ya hapo, sikuwa najua kama anamiliki gari. Lilikuwa ni Toyota Alphard la kisasa, akasema tukitumia ile Noah ya akina Firyaal itakuwa rahisi kutambulika.
Gari tulilopanda lilikuwa na vioo tinted, jambo lililofanya iwe vigumu kwa mtu wa nje kuona kilichokuwa kinaendelea ndani, Junaitha mwenyewe ndiyo akakaa nyuma ya usukani na mimi nikakaa pembeni yake. Kwa jinsi tulivyokuwa tumejikausha, isingekuwa rahisi kwa mtu yeyote kuhisi kwamba kuna mchezo ulikuwa ukiendelea kati yetu.
Hata Shamila mwenyewe, japokuwa mara kwa mara alikuwa akinitazama kwa macho ya kuibia, hakuweza kuhisi chochote, achilia mbali mpenzi wangu Raya ambaye muda wote alikuwa ametulia. Tulitoka na breki ya kwanza ilikuwa ni kwenye kituo kikuu cha polisi, Junaitha akatutaka wote tubaki ndani ya gari, akashuka na kuingia kituoni.
Baada ya kama dakika ishirini, alitoka akiwa ameongozana na askari mmoja aliyekuwa na nyota nyingi mabegani, ambaye alionesha ishara tu, askari zaidi ya sita wenye silaha wakaingia ndani ya difenda, Junaitha akarudi kwenye gari letu na yule askari akaungana na vijana wake.
“Kuna watu itabidi tuwapitie, mwanasheria wetu pamoja na yule mwandishi wa habari, nadhani wote tayari watakuwa wanatusubiri sehemu tuliyokubaliana,” alisema Junaitha. Nikamuuliza swali:
“Kwa hiyo hapa tunaelekea wapi?”
“Tulia jamal, mbona una haraka, nimesema leo ndiyo leo na watu wote watatujua sisi ni akina nani. Shenaiza na Firyaal, naomba mkaze mioyo yenu maana kinachoenda kutokea kwa baba yenu siyo kizuri lakini lazima tufanye hivi,” alisema Junaitha, akawasha gari, tukaondoka huku ile difenda ikitufuata kwa nyuma.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.

5 comments:

 1. hadithi zako zimeishia hewani unaziendelezea wapi?

  ReplyDelete

 2. Mbona hizi hadithi zako haziendelei...Tatizo nini..au unaziendeleza wapi..?

  ReplyDelete
 3. We kaka upo mzima kweli? mbona kimya sanaaa umetuacha hewani tuambie wapi tufatilie hata kama kwa kulipia Thanks

  ReplyDelete
 4. Mini ni mwandishi was riwaya niwapate vipi!?

  ReplyDelete
 5. Mimi ni mwandishi was riwaya niwapate vipi,? Ninayo Kama?
  Doa
  Mbumbumbu
  Salome
  Sikujua
  Chozi la fukara
  Mbio za sakafuni
  Bendera fata upepo
  Elimu ya Samia
  Village doctor
  Mama alisema
  Tafta mchumba
  Ficra potofu
  Mateso ya dada
  Utabiri
  Nikupenini
  Laana
  Wema wangu
  Cheo
  Mdimu
  Sinto oa tena
  Akili kichaka
  Together
  N.k no 0676570495

  ReplyDelete