Thursday, December 21, 2017

VYAKULA VINAVYOONGEZA NGUVU ZA KIUME




Kuongezeka kwa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume kwa vijana na wanaume kumesababisha wengi kuhaha huku na kule kutafuta madawa makali ya kutibu tatizo hilo.
Dawa nyingi za hospitali ambazo hutumika kumaliza au kupunguza tatizo hili, zimebainika kuwa na madhara (side effects) hivyo kusababisha wataalamu kuanza kuhangaika kugundua tiba kwa njia ya vyakula.

CHANZO CHA TATIZO
Tatizo la upungufu wa kiume mara nyingi husababishwa na matatizo ya kimwili au ya kisaikolojia ambapo mwanaume huwa dhaifu wakati wa tendo na wakati mwingine kushindwa kabisa kufanya chochote.

Sababu za kimwili (Physical) zinaweza kuwa ni kwa sababu mishipa ya damu inashindwa kufikisha damu yenye msukumo kwenye viungo vya uzazi.

Kuongezeka kwa kiwango cha mafuta mwilini husababisha mafuta hayo kuganda kwenye kuta za mishipa ya damu na kuzuia damu kutiririka vizuri, tatizo ambalo kitaalamu huitwa atherosclerosis.

Pia wagonjwa wa kisukari nao wapo kwenye hatari kubwa ya kukumbwa na tatizo hili. Upungufu wa madini ya Zinc na vitamin pia husababisha tatizo hili.

Sababu za kisaikolojia ni pamoja na kuwa na msongo wa mawazo, hofu, uchovu wa akili au kama mtu aliwahi kukumbwa na tatizo kubwa siku za nyuma ambalo limemuathiri kisaikolojia au kama ana dosari katika mfumo wake wa homoni.

Sababu nyingine zinazoweza kusababisha tatizo hili ni matumizi ya madawa ya kulevya, pombe au kuchanganya vyote viwili kwa pamoja. Uvutaji wa sigara nao ni sababu nyingine ya tatizo hili, pamoja na kuendesha baiskeli kwa muda mrefu.

VYAKULA VINAVYOSAIDIA KUMALIZA TATIZO

Vyakula ambavyo vimethibitishwa kitaalamu kwamba vina uwezo wa kumuongezea mwanaume nguvu za kiume ni pamoja na:

1. Vitunguu swaumu
Vitunguu hivi vinaelezwa kuwa na kirutubisho kiitwacho allicin ambacho huongeza msukumo wa damu kuelekea kwenye viungo vya uzazi.

2. Ndizi mbivu
Inaelezwa kuwa ndizi mbivu zina kirutubisho kiitwacho bromelain ambacho husaidia kuupa mwili nguvu wakati wa tendo, kuongeza msukumo wa damu kwenye viungo vya uzazi na kuongeza hamu ya kufanya tendo. Pia ndizi zina Vitamin B ambayo huupa mwili nguvu.

3. Karanga
Mbali na kuwa na mafuta mengi, karanga zina virutubisho viwili muhimu, Amino Acid na L-Arginine ambavyo humuongezea mwanaume nguvu wakati wa tendo na kuchochea uzalishwaji wa mbegu za kiume na kuongeza hamu ya tendo.


4. Chocolate
Chocolate zina vichocheo vya phenylethylamine na alkaloid ambavyo huongeza mhemko wakati wa tendo. Pia huongeza nguvu kwa wanaume hivyo kuleta ufanisi wakati wa kufanya mapenzi.

5. Kunazi (Blueberries)
Haya ni matunda madogomdogo jamii ya zabibu ambayo huliwa na binadamu. Matunda haya yanaelezwa kuwa na nguvu kama ilivyo dawa ya Viagra. Tafiti za kitaalamu zinaeleza kuwa matunda haya yana vichocheo ambayo hulaainisha mishipa ya damu na kufanya damu isambae kwa kasi kuelekea kwenye viungo vya kiume.

Pia matunda haya yana kambalishe (fiber) ambayo huyeyusha lehemu (cholesterol) kwenye mishipa ya damu na kuitoa nje ya mwili kabla haijaleta madhara kwa binadamu hivyo kuongeza ufanisi wakati wa tendo.

6. Pilipili
Pilipili zinao uwezo mkubwa wakumaliza tatizo hili. Unaweza kuchanganya kwenye chakula au ukala hivyohivyo kwa kutafuna kiasi kidogo mara kwa mara. Pilipili zina virutubisho ambavyo husaidia kuufanya mzunguko wa damu uwe mkubwa na kuamsha hisia kali za mapenzi.

7. Pweza na chaza
Aina hizi za viumbe wa baharini, huwa na madini ya zink na chumvi ambayo yanatajwa kusaidia uzalishaji wa vichocheo vinavyohamasisha msisimko wa mwili wakati wa tendo la ndoa. Jenga utaratibu wa kunywa supu ya pweza mara kwa mara na matokeo yake utayaona.

8. Parachichi
Parachichi lina uwezo mkubwa wa kuzalisha vitamini E ambayo husaidia katika uzalishaji wa homoni za kiume. Inatajwa kuwa watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwa na msisimko mkubwa wa kimapenzi.


8. Tikitimaji
Matunda haya pia yana uwezo mkubwa wa kuongeza nguvu za kiume. Wengi hufanya makossa wanapokula matunda haya kwa kutema mbegu zake. Tikiti linapaswa kuliwa pamoja na mbegu zake, angalau vipande viwili au vitatu kwa siku.

9. Maji
Maji safi ya kunywa, yanatajwa pia kuwa na uwezo mkubwa wa kusafisha mwili, hasa mfumo wa uzazi na kukupa nguvu za kufanya tendo la ndoa. Unapaswa kunywa maji kwa wingi lakini pia, kila mkojo unapokubana, ni muhimu kwenda kuutoa kwani kukaa na mkojo kwa muda mrefu, husababisha baadhi ya misuli ambayo ni muhimu kwenye tendo, kulegea.

10. Komamanga
Haya ni aina fulani ya matunda, ambayo ndani yana mbegu nyekundu. Komamanga linatajwa kuwa na virutubisho muhimu vya kusisimua misuli na kuamsha hisia za kushiriki tendo la ndoa.

11. Mvinyo mwekundu
Mvivyo mwenyekundu unatajwa kuwa na uwezo wa kuuchangamsha mwili na kuongeza msukumo wa damu, kiasi cha kumuondolea mtu uchovu kabla na baada ya tendo la ndoa. Pia unatajwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuamsha hisia baada ya kumaliza raundi ya kwanza ya tendo la ndoa.

12. Mbegu za maboga
Mchangayiko wa mbegu mbalimbali, hasa za maboga huongeza nguvu na ufanisi wa kufanya tendo la ndoa.



1 comment:

  1. Nimeenjoy na elimu yako nzuri aiseeee,Kuna siku nilikunywa Tanzania kinyagi mizinga midogo mbili ya 4000 nikimix na soda Aina ya Fanta manzee mashine haikusimama na ikisimama inakuwa legelege,ndo maana ikabidi nitembelee hii page nipate maarifa sbb hii Hali haikuwwa ya kawaida kwangu,Tangia siku hiyo nazichukia pombe Kali walai

    ReplyDelete

THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 1

Mtunzi: Hashim Aziz (Hashpower) 0719401968 “Ngo! Ngo! Ngo! Fungua!” “Nanii?” “Fungua!” “Jitambulishe kwanza, wewe nani?” “Nimese...