Tuesday, January 6, 2015

IDI AMINI DADA; MAMBO 10 USIYOYAJUA KUHUSU

Wengi wanamkumbuka kutokana na ukatili wake kipindi alipokuwa madarakani na vita kali ya kugombea mpaka iliyopiganwa kati ya nchi yake ya Uganda dhidi ya Tanzania, enzi hizo ikiwa chini ya Rais Julius Kambarage Nyerere.
Anaitwa Idi Amini Dada, Rais wa tatu wa Uganda aliyeingia madarakani baada ya kumpindua Rais Milton Obote na yafuatayo ni mambo kumi usiyoyajua kuhusu dikteta huyu.
1. Katika kipindi alichokuwa madarakani, kutoka 1971 hadi 1979, inakadiriwa kwamba aliwaua kikatili zaidi ya watu laki tano waliokuwa wakienda kinyume na amri zake.

2. Aliwahi kuwa mwenyekiti wa OAU (Organisation of African Unity) na alikuwa na ndoto za kuiunganisha Afrika kuwa nchi moja ili aitawale, kama alivyokuwa akiwaza rafiki yake mkubwa, Muammar Gaddafi.
3. Alikuwa na elimu ndogo aliyoipata kwenye Shule ya Kiislamu ya Bombo na inaelezwa kuwa baadaye aliacha shule akiwa hajui vizuri kuandika wala kusoma.
4. Mpaka anakufa, historia ya maisha yake haikuwa ikifahamika vizuri. Wachambuzi wanaeleza kuwa alizaliwa Koboko mwaka 1925, kutoka kabila la Kakwa.

5. Inaelezwa kuwa baada ya kuzaliwa, baba yake mzazi, Andreas Nyabire alimtelekeza, akalelewa na mama yake mashambani, Kaskazini Magharibi mwa Uganda mpaka alipokuwa mkubwa.
6. Baada ya kupinduliwa na majeshi ya Tanzania mwaka 1978, alikimbilia Libya alikopewa hifadhi na Gaddafi na baadaye kukimbilia Saudi Arabia alikofia kwa maradhi ya figo Agosti 16, 2003.
7. Alijiunga na jeshi la mkoloni, King's African Rifles (KAR) mwaka 1946 akiwa mpishi msaidizi. Akawa anapanda vyeo taratibu hadi alipofikia ngazi ya luteni mwaka 1961, akiwa mtu mweusi wa pili kufikia cheo hicho. Akaendelea kupanda hadi alipojitangaza kuwa Field Marshal kabla ya kupinduliwa.
8. Mbali na mambo ya jeshi na siasa, Amini alikuwa mwanamichezo mashuhuri ambapo alikuwa akipigana masumbwi na pia alikuwa muogeleaji.
9. Idi Amini alikuwa na wake zaidi ya watano na jumla ya watoto 40. Mwaka 1974, aliwapa talaka wake zake watatu, Malyamu, Nora na Kay kwa wakati mmoja na kuoa wengine.
10. Kulikuwa na tetesi za muda mrefu kuwa Amini alikuwa akila nyama za watu na inadaiwa kuwa, mkewe mmoja ambaye mpaka leo hafahamiki alipo, Nora aliuawa na kuliwa nyama na mumewe baada ya kupewa talaka ingawa hakuna ushahidi wa kutosha.

No comments:

Post a Comment

THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 1

Mtunzi: Hashim Aziz (Hashpower) 0719401968 “Ngo! Ngo! Ngo! Fungua!” “Nanii?” “Fungua!” “Jitambulishe kwanza, wewe nani?” “Nimese...