Monday, August 6, 2012

KEAGAN ANYAKUA DOLA 300,000 BBA STARGAME

HASH POWER 7113


Johannesburg, Afrika Kusini
Lile shindano lililowabamba watu kibao ndani na nje ya Bara la Afrika la Big Brother Africa ‘Stargame’, Jumapili iliyopita lilifikia tamati ambapo mshiriki kutoka Sauzi, Keagan Petersen aliibuka kidedea na kunyakua kitita cha dola 300,000 (zaidi ya Sh. Milioni 450) huku Prezoo kutoka Kenya akishika nafasi ya pili.
Kwa mujibu wa wadau waliokuwa wanalifuatilia shindano hilo, Prezoo aliyekuwa na nafasi kubwa ya kuibuka kidedea, ameponzwa na tabia yake ya kucheza na mioyo ya mabinti mjengoni, kutokuwa mkweli kwenye mapenzi kama ilivyotokea kwa Goldie na kupenda ugomvi na ulevi wa kupindukia, mambo yaliyompunguzia mashabiki na hivyo kukosa kura nyingi.
Hata hivyo, licha ya kushika nafasi ya pili, Prezoo amelamba dili la nguvu la kuwa balozi wa Kampeni ya ONE na kupata zali la kwenda kuhudhuria shoo ya Jay Z nchini Marekani siku chache zijazo.
Washiriki kutoka Tanzania, Hilda na Julio walitolewa katika hatua ya kwanza ya mtoano na kusababisha Watanzania wengi wasiendelee kufuatilia shindano hilo.
 

No comments:

Post a Comment

THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 1

Mtunzi: Hashim Aziz (Hashpower) 0719401968 “Ngo! Ngo! Ngo! Fungua!” “Nanii?” “Fungua!” “Jitambulishe kwanza, wewe nani?” “Nimese...