Friday, July 20, 2012

TAARIFA YA RAIS KIKWETE KUFUATIA AJALI YA KUZAMA KWA MELI YA MV SKAGIT

JANA tarehe 18 Julai, 2012, majira ya alasiri kumetokea ajali ya kuzama kwa meli ya MV SKAGIT katika eneo la Chumbe, Zanzibar. Meli hiyo iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kueleka Zanzibar ilikuwa imebeba watu 290. Kati yao watu wazima 250, watoto 31 na wafanyakazi wa meli 9. Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete aliagiza vyombo vya ulinzi na usalama vya Serikali ya Muungano yaani JWTZ na Polisi waanze kazi ya uokoaji mara moja. Kazi hiyo imefanywa kwa kushirikiana na vyombo vya usalama vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na meli za makampuni binafsi. Mpaka giza lilipokuwa limeingia na hivyo kazi ya uokoaji kusitishwa mpaka kutakapokucha tarehe 19 Julai, 2012, watu 136 walikuwa wameokolewa na maiti 31 zilikuwa zimepatikana. Aidha, mali zilizokuwa kwenye meli hiyo hazikuweza kuokolewa. Kufuatia ajali hiyo, Rais wa Jamhuri ya Muungano alizungumza na Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Alimpa pole kwa ajali iliyotokea hasa kwa vifo na majeraha waliyopata Watanzania wenzetu na watu wasiokuwa raia wa Tanzania.

Wednesday, July 18, 2012

SKAGIIT YAZAMA BAHARI YA HINDI

HASH POWER 7113
Boti ya Skagit inayomilikiwa na Kampuni ya Seagul iliyokuwa inasafiri kutoka Dar es Saalam kwenda Zanzibar ikiwa na abiria zaidi ya 290 imezama kwenye bahari ya Hindi, eneo la Chumbe na kusababisha maafa makubwa baada ya kile kilichoelezwa kuwa ni injini za boti hiyo kuzimika ghafla.
 
Mmoja wa majeruhi wa ajali ya meli ya MV Skagit iliyozama katika eneo la Pungume karibu kilomita 48 kutoka Bandari ya Zanzibar jana, akipata matibabu.
 Majeruhi wakizidi kupatiwa huduma ya kwanza baada ya ajali hiyo.
...Huduma za matibabu zikiendelea.
Majeruhi wakiwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja.
(Picha kwa hisani ya http://issamichuzi.blogspot.com/)

Sunday, July 1, 2012

MKASA WA WAHAMIAJI HARAMU KUTOKA ETHIOPIA

HASH POWER 7113// ACREDITATION; This Day Magazine, Michuzi Blogs


 Baada ya kibali cha kuwazika nchini Tanzania wahamiaji toka Ethiopia waliofariki ndani ya lorry walilokuwa wanasafiria kutolewa na Serikali yao  ya Ethiopia, Serikali ya Tanzania iliamua mazishi ya Raia hao wa Ethiopia kufanyika Juni 29, 2012 Alasiri Mkoani Dodoma na Morogoro kwa baadhi ya miili iliyokuwa imehifadhiwa hospitali ya Mkoa Morogoro na kazi inayoendelea hapa ni ya uchimbaji wa makaburi.
 Vijana 84 wahamiaji kutoka Ethiopia walionusurika kifo wakipita mmoja baada ya mwingine wakitoa heshima zao za mwisho na kuwaaga ndugu zao kwa kutupa udongo kwenye makaburi yaliyohifadhi miili ya wenzao waliopoteza maisha katika tukio la kusafirishwa kwenye Lorry.
 Kijana Chafamo Yosef (kulia) Muamiaji raia wa Ethiopia akitoa neno la shukrani muda mfupi baada ya kumalizika kwa mazishi kwa jinsi ambavyo wamepatiwa msaada na serikali ya Tanzania tangu siku walipokutwa wametelekezwa, miongoni mwa vitu alivyoahidi akifika nchini kwao Ethiopia ni kuwaelezea watu wa Ethiopia kuwa walidanganywa na kusababishiwa matatizo makubwa hadi baadhi yao kupoteza maisha lakini wao Mungu amewanusuru, wameona nchi nzuri ya Tanzania, wamekutana na serikali nzuri iliyowahudumia kila kitu, na wananchi wenye mioyo ya huruma na ukarimu.
 Raia wahamiaji kutoka Ethiopia walionusurika kifo wakiwa wameinamisha vichwa vyao chini kuwaombea sala wenzao waliopoteza maisha wakati wa shughuli ya mazishi.
 Safari ya mwisho ya kuwasindikiza na kuwahifadhi katika nyumba zao za milele wahamiaji 43 (21 Dodoma, 23 Morogoro) kutoka Ethiopia waliopoteza Maisha ilihitimishwa kwa kazi ya kufukia makaburi iliyofanywa na vijana na wananchi mbalimbali waliojitokeza kwenye mazishi hayo.
 Wahamiaji hawa (walionusurika) wamekuwa watu waliozamia katika sala na maombi baada ya kunusurika kifo ukizingatia baadhi ya wenzao walikufa katika tukio hilo, kila baada ya chakula jioni wanapewa muda wa kufanya maombi.

 Wahamiaji kutoka Ethiopia walipatiwa kila aina ya msaada wa muhimu uliohitajika kwa wakati kama malazi, mavazi, chakula dawa,  matibabu ya kisaikolojia nk
 Mtoa huduma ya kwanza wa Msalaba Mwekundu akimfunika mmoja wa wahamiaji kutoka Ethiopia ambaye alikuwa na tatizo la maumivu kifuani.
Mabaki ya vitu, miongoni mwake chupa za maji zikiwa nyingi na vifurushi vya sukari na mikate ambavyo walikuwa wanatumia wahamiaji hao kama chakula kwa ajili ya kujinusuru uhai wakiwa ndani ya lorry lililowasafirisha likiwa limefunwa pande zote bila kuruhusu hewa kupita, masalia haya badae yaliteketezwa moto.
 Vijana walioandaliwa kwa ajili ya shughuli ya Mazishi wakishusha miili ya Marehemu kwenye nyumba zao za milele (makaburi) ikiwa ni hatua za mwisho za kuhitimisha safari ya mwisho ya kuwapumzisha watu hao waliopoteza maisha.
 Vijana Wahamiaji kutoka Ethiopia walionusurika kifo wakilia kwa uchungu muda mfupi baada ya miili ya Wenzao waliopoteza maisha kuwasili eneo la maziko mjini Dodoma, jumla ya Waethiopia 43 walipoteza maisha ambapo 21 wamezikwa Dodoma na 23 Morogoro.
Vijana Wahamiaji kutoka Ethiopia walionusurika kifo wakiwa wamejipanga mistari miwili wakionekana wenye huzuni muda mfupi baada ya kuwasili eneo lililoandaliwa katika Manispaa ya Dodoma kwa ajili ya kuwazika wenzao waliopoteza maisha katika tukio hilo la kusikitisha, jumla ya Waethiopia 43 walipoteza maisha ambapo 21 wamezikwa Dodoma na 23 Morogoro.
 Picha zote na Jery Mwakyoma
Kwa hisani ya Michuzi Blog

THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 1

Mtunzi: Hashim Aziz (Hashpower) 0719401968 “Ngo! Ngo! Ngo! Fungua!” “Nanii?” “Fungua!” “Jitambulishe kwanza, wewe nani?” “Nimese...