Saturday, January 14, 2012

MTOTO WA LIYUMBA, WENZAKE WAKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA

Sehemu ya shehena ya madawa yaliyokamatwa
(Kwa msaada wa Michuziblogspot.com)
Jumla ya kilo 209 za dawa za kulevya aina ya Heroine zinazokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 9, zimekamatwa katika Kijiji cha Mchinga mkoani Lindi na watu … wanashikiliwa na jeshi la polisi kuhusiana na dawa hizo haramu.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Kamanda wa Polis wa Mkoa wa Lindi, George Mwakajinga, aliwataja waliokamatwa kuwa ni Morine Amatus Liyumba (21),
Pendo Mohamed Cheusi (67) ambaye ni mkazi na mkulima katika kijiji hicho, Hemed Said (27), dereva na mkazi wa Mtoni, jijini, Dar es Salaam, Ismail Adam (Athuman Mohamed Nyaubi ,28,) ambaye ni mfanyabiashara wa magari jijini Dar es Salaam.

Inaelezwa kuwa kiwango walichokamatwa nacho, ni kikubwa na hakijawahi kutokea katika historia tangu kuanzishwa kwa kitengo cha kupambana na kuzuia dawa za kulevya nchini mwaka 1990. Shehena hiyo iliyokuwa imefichwa kitaalamu ndani yamadumu makubwa, inadaiwa kuwa ilikuwa ikisafirishwa kuelekea nchini Afrika Kusini. Watuhumiwa walisafirishwa hadi jijini Dar es Salaam na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani siku chache zijazo kujibu tuhuma zinazowakabili.

No comments:

Post a Comment

THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 1

Mtunzi: Hashim Aziz (Hashpower) 0719401968 “Ngo! Ngo! Ngo! Fungua!” “Nanii?” “Fungua!” “Jitambulishe kwanza, wewe nani?” “Nimese...