Saturday, September 10, 2011

MELI YA SPICE YAZAMA, WATU 2000 WAHOFIWA KUFA

Meli ya Spice ikizama. Picha kwa hisani ya Jamii Forum
HASH POWER 7113// Acreditation: Jamii Forum
Meli ya Mv Spice Islander iliyokuwa inasafiri katika Bahari ya Hindi kwenye mkondo wa Nungwi kutoka Bandari ya Malindi, Unguja kuelekea Wete, Pemba, saa 4 usiku wa Septemba 9, 2011 imezama na watu zaidi ya 2,000 wanahofiwa kupoteza maisha.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo, baada ya meli kufika eneo la mkondo bahari wa Nungwi, ilianza kupata misukosuko kabla ya kuanza kuzama kiubavu. saa 8 za usiku.

Mpaka sasa, kwa mujibu wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya makamu wa Rais, Mohamed Aboud Mohamed, majeruhi zaidi ya 250 tayari wameokolewa na kusafirishwa kwa boti ziendazo kasi mpaka kwenye Bandari ya Malindi, Unguja ambapo watapelekwa kwenye Viwanja vya Maisra. Juhudi za kuokoa miili na majeruhi wengine zinaendelea kwa kutumia helikopta mbili za jeshi. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Ali Mohamed Shein yuko eneo la tukio kujionea hali halisi.

Taarifa zaidi zitazidi kuwajia kupitia hapahapa. Stay tuned.
Kwa (hakuna mwenye idadi kamili lakini namba hiyo ndio inayotajwa)

Sasa wakati janga kama hili linatokea huwa kunakuwa na idadi mbali mbali zinatolewa lakini mimi nimeambiwa namba hiyo na watu wa 5 tofauti toka sehemu mbali mbali kuanzia bandarini mpaka waliosindikiza jamaa zao ila kama namba kamili ikiletwa na serikali basi tutarekebisha tuu hivyo tunaomba coordination ya members na subra kwani hatuna taarifa kamili

  • Meli ilianza kuzama kiubavu na imechukua muda kuzama.
  • Inasemakana (from redio na jamaa wa ISTIQAMA) sababu ilikuwa imejaa mizigo na abiria.
  • Abiria wengi walikuwa ni watoto na wazazi wao ambao walienda Unguja kula IDDI na walikuwa wanarejea kwani skuli zingine zafunguliwa next week
  • Kawaida Unguja meli huwa zinaondoka Gatini zikishapakia na kukaa nje huko karibu na kati ya bahari mpaka muda ndio safari zinaanza
  • Watu waliokolewa (sijajua na nani) taarifa ninazopewa ni kuwa hawafiki 25 (tutajua namba kamili kadri muda unavyozidi kwenda)
  • watu wengi walikuwa watoto waliokwenda Unguja kula Iddi na walikuwa wanarejea kwani wiki ijayo baadhi ya skuli zafunguliwa
  • As I write kuna mmoja kati ya mabaharia kasimama juu ya meli ambayo inazama na anasema mawasiliano yanaweza kukatika at anytime kwani naye anaweza kuzama
  • Kama ZANTEL au vyombo vya habari na mawasiliano wanauwezo wawasiliane na idara za uokozi kama JWTZ ili wapeleke helicopeter zao za kuokoa.
  • Lakini mtu kama KETAN na wengineo anaweza kutoa helicopter zake atoe wakiokolewa hata watoto 20 si haba ni uhai
  • Inasemekana kuwa speed boats zingine zinaelekea eneo la tukio

Point of notice:
Daftari la idadi ya abiria halipo so haijulikani wangapi wamo mle japo namba ni hiyo 2,000 sasa nadhani kwa mpango huo na kwa namna tunavyo operate kikawaidaitakuchukua siku kadhaa kujua namba halisi (kama daftari na copy za risiti hazitopotea)


Tunaomba updates coordination toka kwenye websites za:

JWTZ
JESHI LA POLISI
OFISI YA WAZIRI MKUU
WIZARA YA USAFIRISHAJI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI

mwenye habari zaidi tunaomba kama kutakuwa mwenye nafasi aanzishe facebook au social network pages atupe updates. Mwanakijiji hebu wacheki CNN, Invisible akiamka na wenzie watauleta updates zaidi

Najua haikatulia lakini nadhani anyone can post updates hapo au namba za simu au lolote bas tuendelee kuhabarishana.

InshaAllah nitaendelea kuwahabarisha kadri muda unavyozidi kwenda

Inna Lillahi wa Inna illahi Rajuu'n

No comments:

Post a Comment

THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 1

Mtunzi: Hashim Aziz (Hashpower) 0719401968 “Ngo! Ngo! Ngo! Fungua!” “Nanii?” “Fungua!” “Jitambulishe kwanza, wewe nani?” “Nimese...