Tuesday, July 12, 2011

MKOLONI AANZA KUIPROMOTI KAULI BILA VITENDO

HASH POWER 7113// Acreditation: Deiwaka Entertainments
Mkoloni

Staa wa crew ya Wagosi wa Kaya, Fred Malik ‘Mkoloni’ ameamua kuwa ‘siriaz’ kuipromoti ngoma yake inayokwenda kwa jina la Kauli Bila Vitendo.
Mkoloni ambaye kwa sasa ni Katibu wa Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ alisema na ripota wetu kuwa ameona ngoma yake haiendi sawa, kwa hiyo ameongeza juhudi katika kuipa promo.

“Nataka niisambaze mikoa yote na kwenye redio za watu ambao wanajua nini maana ya sanaa na ujumbe. Lengo ni Watanzania wapate ‘meseji’, waone jinsi serikali yetu ilivyo na uhodari wa kauli bila vitendo,” alisema Mkoloni.

Mkoloni ambaye amehamia Mbeya kwa sasa alisema: “Nipo nafanya kazi za wananchi kuhakikisha mipango ya mbunge inatekelezwa yote kama alivyoahidi. Kuna miradi mingi naisimamia lakini muziki upo pale pale na Anti Virus Volume II inakuja.”

No comments:

Post a Comment

THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 1

Mtunzi: Hashim Aziz (Hashpower) 0719401968 “Ngo! Ngo! Ngo! Fungua!” “Nanii?” “Fungua!” “Jitambulishe kwanza, wewe nani?” “Nimese...