Tuesday, September 7, 2010

NJIA ZA UZAZI WA MPANGO

Ili watoto wakue vizuri baada ya kuzaliwa, ni lazima wapate mahitaji muhimu na ya lazima, ikiwemo kunyonyeshwa maziwa ya mama kwa muda unaostahili, kupatiwa chakula bora, huduma bora za afya, malazi, mavazi nk.
Kwa kawaida mtoto mchanga anapaswa kunyonyeshwa kwa muda wa miaka miwili kabla ya kuachishwa kunyonya. Endapo mwanamke atapa ujauzito mwingine wakati bado ananyonyesha, itasababisha mtoto akatishwe ziwa kabla ya muda muafaka, hali ambayo ina madhara makubwa ya kiafya kwa mtoto na mama.

Zifuatazo ni mbinu mbalimbali za kisasa za uzazi wa mpango (Family planning and contraception) zinazoweza kutumika kupanga familia bora na ya kisasa:


1. KUFUNGA UZAZI (VASECTOMY AND TUBAL LIGATION)
Hii ni mbinu inayopaswa kutumiwa na wanandoa au wenzi ambao tayari wamepata idadi ya watoto waliokuwa wanawahitaji. Kwa wanaume, kitendo cha kufunga uzazi huitwa Vasectomy na huhusishwa kukatwa, kutenganishwa na kisha kufungwa kwa mirija ya kupitishia mbegu za kiume (Vans deferens) na kufanya mbegu za kiume (Sperm zisiwe na uwezo wa kufika ukeni).
Kwa wanawake, kitendo cha kufunga uzazi huitwa Tubal ligation na huhusisha kukatwa na kufungwa kwa mirija ya kusafirishia mayai ( Oviduct) na hivyo kuzuia mayai kushindwa kufika kwenye mji wa uzazi (Uterus).

FAIDA
Mbinu hii haiathiri uwezo wa wenzi kufanya tendo la ndoa na ni salama kwa asilimia 100.
Huhusisha mwanandoa mmoja tu, kama baba au mama akifunga uzazi hakuna haja ya mwenzake naye kufunga.
Hakuna madaliko yoyote yanayoweza kuonekna kwa macho kwenye viungo vya uzazi.

MADHARA
Huhusisha upasuaji mdogo ambao huwa na maumivu kiasi.
Ukifunga uzazi huwezi tena kurudi katika hali yako ya awali kwa maisha yako yote yaliyosalia.

2. VIDONGE VYA UZAZI WA MPANGO ( ORAL CONTRACEPTIVES)
Vidonge vya uzazi hutengenezwa vikiwa na homoni ambazo hufanya kazi sawa na homoni za asili zilizoko ndani ya mwili wa mwanamke. Vidonge hivi vinapotumiwa, huingia ndani ya mzunguko wa damu na kufanya kazi ya kuzuia upevushwaji wa mayai ya kike kwa kuzuia uzalishwaji wa homoni ya FSH (Follicle stimulating hormone) kutoka kwenye tezi ya pituitary, pia kuzuia homoni za Oestrogen na Progesteron kufanya kazi yake na hivyo kufanya kitendo cha kutunga mimba kisiwezekane.

FAIDA
Zikitumiwa vizuri kulingana na maelezo ya daktari, huweza kuzuia mimba kwa asilimia 99.
Hutumiwa na wanamke tu.

HASARA
Vidonge hivi vikitumiwa kiholela huwa na madhara makubwa, ikiwemo kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi, damu kuganda katika mji wa mimba (Uterus), kuongezeka kwa uzito, matiti kuwa makubwa na kulegea, kupata kichefuchefu cha mara kwa mara na kupungua kwa uwezo wa mwanamke kubeba ujauzito pindi atakapohitaji mtoto.

3. KITANZI (INTRA- UTERINE DEVICE)
Katika mbinu hii ya uzazi wa mpango, kifaa maalum (Kitanzi ) huingizwa ukeni na kusukumwa mpaka kwenye mji wa mimba(Uterus). Kitanzi hufanya kazi ya kuzuia mimba kutungwa kwenye kuta za mji wa uzazi kwa kuzuia yai la kike kukutana na mbegu za kiume.

FAIDA
Ikitumiwa ipasavyo kulingana na maelezo ya kitaalamu ya daktari, huzuia mimba kwa asilimia 96.

HASARA
Kitanzi kinaweza kutoka chenyewe hasa kama mwanamke anafanya shughuli ngumu.
Kitanzi huweza kusababisha michubuko yenye maumivu kwenye kuta za mji wa uzazi au kuharibu kabisa kizazi. Pia husababisha damu kutoka ovyo sehemu za siri kutokana na michubuko kwenye kuta za mji wa mimba (Uterus)
Itaendelea wiki ijayo

No comments:

Post a Comment

THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 1

Mtunzi: Hashim Aziz (Hashpower) 0719401968 “Ngo! Ngo! Ngo! Fungua!” “Nanii?” “Fungua!” “Jitambulishe kwanza, wewe nani?” “Nimese...