Monday, August 2, 2010

WAGHANA KUITEKA NOLLYWOOD


Lagos- Nigeria
Idadi ya wasanii kutoka nchini Ghana wanaofanya vyema katika kiwanda cha filamu cha Nigeria, Nollywood wanazidi kuongezeka kwa kasi, huku wakitishia kuliteka soko la filamu Nigeria na Ghana. Katika siku za hivi karibuni, wasanii kama Jackie Appiah, Van Vicker, Nadia Buari, Majid Mikel na wengineo, wameonekana kung’ara kwa sana Nollywood, huku ustaa wa baadhi ya wasanii wazawa wa Nigeria ukianza kusuasua.

Hali hiyo imezua mivutano ya hapa na pale baina ya wasanii wa Nollywood na Ghollywood, ambapo Wanigeria wanawataka wasanii kutoka Ghana wakafanyie kazi zao nyumbani kwao ili kuinua kiwanda chao cha Ghollywood, na sio kuzamia Nigeria kwani wanawazibia riziki zao. Kauli hiyo imepingwa na baadhi ya wasanii wa Ghana, ambao wameeleza kuwa katika kipindi hiki cha mapinduzi ya kiteknolojia, ni lazima wasanii wajaribu kutafuta maisha sehemu nyingine nje ya mipaka yao, na kuwataka wasanii wa Nigeria kuhamia Hollywood kama wanaona Nollywood kumevamiwa na Waghana.

No comments:

Post a Comment

THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 1

Mtunzi: Hashim Aziz (Hashpower) 0719401968 “Ngo! Ngo! Ngo! Fungua!” “Nanii?” “Fungua!” “Jitambulishe kwanza, wewe nani?” “Nimese...