RIHANNA NDANI YA SKENDO YA USAGAJIMwanadada Robyn ‘Rihanna’ Fenty kwa mara nyingine anamake headlines katika magazeti na mitandao mbalimbali ya kiwanja, akihusishwa na scandali ya mapenzi ya jinsia moja. Katika wimbo wake wa Te Amo, ukifuatilia kwa makini kuanzia mashairi yake, hadi video yake, Rihanna anaonekana kuyafagilia mapenzi ya jinsia moja, huku picha za video zikimuonesha akiwa amezama kwenye mahaba na mwanamke mwenzake, hali ambayo inazua utata mkubwa kuhusiana na mwenendo wake wa kimapenzi, hususan baada ya kutengana na Chriss Brown, aliyekuwa king’ast wake.

Miongoni mwa mashairi yanayoonekana kusifia usagaji, ni pale alipoelezea namna mwanamke mwenzake alivyomshika kiuno na kumkumbatia, kisha wakawa wanachezeana kwenye mwanga hafifu wa mshumaa. Rihanna anasikika akizidi kueleza kuwa mapigo ya moyo yalikuwa yakimwenda mbio na akajihisi yuko kwenye sayari nyingine. Kama hiyo haitoshi, siku za hivi karibuni Rihanna aliripotiwa na mtandao mmoja wa nchini Marekani, kuwa alionekana akinunua vifaa vinavyofanana na viungo bandia vya uzazi vya kiume (Sex toys) kutoka kwenye duka moja huko jijini New York, ingawa mwenyewe alikanusha vikali tuhuma hizo.

No comments:

Post a Comment