NOLLYWOOD; TAMAA YA PESA INAIMALIZA NOLLYWOOD- DURU

Abuja- Nigeria
Msanii Francis Duru, ambaye alipotea kwenye game kwa takribani miaka kumi, amerudi upya huku akisisitiza kuwa uroho wa pesa na tamaa kali walizonazo wasanii wa filamu , madairekta na wadau mbalimbali wa filamu, ndiyo sababu kubwa iliyomfanya aipe kisogo sanaa hiyo kwa muda. Msanii huyo aliyewahi kutesa katika movie ya Total War, Final War, alisema kuwa aliamua kufanya shughuli zake binafsi na kusimama kwa muda kucheza muvi, baada ya kuchoshwa na tamaa za wadau wa filamu nchini Nigeria, ambapo msanii anaambulia maslahi kiduchu kutokana na uroho wa pesa wa wadau wanaopewa jukumu la kusimamia malipo ya filamu.

Duru ambaye anamiliki kampuni yake binafsi inayojihusisha na masuala ya burudani, amewasihi wadau wa filamu kuwa na nidhamu ya pesa, hasa za wasanii wanaoshiriki kucheza movie, na kwamba kama wadau hawatajirekebisha, wasanii ambao ndiyo injini ya Nollywood, watakata tamaa na hicho kitakuwa kikwazo kikubwa kwa tasnia ya filamu nchini humo na huenda
Nollywood ikapoteza kabisa hadhi yake iliyonayo kwa sasa.

No comments:

Post a Comment