Saturday, August 28, 2010

LETS TALK ABOUT LOVE!

Sababu kumi za kusema ‘Nakupenda’
NENO “nakupenda” linaweza kumaanisha kila kitu kwa mtu fulani unayemwambia hivyo. Kwa upande mwingine, uhusiano unapozidi kuendelea kati ya watu, kutokana na mazoea kuna wakati mtu anaweza kusahau kulisema neno hilo. Hata hivyo, kumwambia mtu “nakupenda” kunasaidia kuendeleza uhusiano wa karibu na mtu huyo kwa muda mrefu. Hivyo, pamoja na kuonekana kwamba linaweza kuwa na maana moja, neno “nakupenda” ni pana zaidi katika mahusiano, kwani linajumuisha mambo yafuatayo:


Upendo
Ni wazi kwamba sababu ya kusema “nakupenda” ni kwa sababu mtu unayemwambia hivyo unakuwa unampenda kweli. Kulitamka neno hili kunaweza kutokana na kukumbuka kitu fulani ulichowahi kutendewa na mtu fulani, na hivyo kujikuta ukimwambia moja kwa moja kwamba unampenda.

Uhakikisho
Mtu anaposikia kuambiwa neno hilo ni kweli hujisikia unampenda na kwamba unamtilia maanani. Hivyo, mtu unayekuwa naye kwa muda mrefu akawa hajalisikia neno hilo kutoka kwako, ataanza kuingiwa na woga kwamba huenda kumpendi tena.
Fursa ya kujieleza
Neno hilo linatoa fursa ya kuelezea hisia zako kwa uhuru, kwani unaweza usipate fursa hiyo tena. Dunia inaweza kubadilika na ukakosa kabisa fursa ya kulisema kwa watu wengine.
Usalama
Mtu anapolisikia neno “nakupenda” hujiona yuko salama zaidi katika mahusiano na mtu wanayehusiana naye. Kwani atazifahamu hisia zako na yeye kujua msimamo wake.
Kukutanisha watu
Hutumika katika kuwakutanisha wapenzi waliokuwa “wamepoteana” kwa muda. Hivyo kumwambia kwamba unampenda unakuwa unamvuta karibu yako na hivyo kumtoa mashaka yoyote aliyokuwa nayo.
Kumwelewa mwenzako
Unaposema “nakupenda”, mara nyingi unategemea kupata jibu kutoka kwa yule unayemwambia. Hata kama ulikuwa unajihisi mpweke au kuwa na wasiwasi katika uhusiano na mtu fulani, kulitamka neno hilo ni dhahiri litakufanya upate uhakika kwamba uliyemwambia hivyo atatoa jibu kwa njia yoyote. Hivyo, hali hii itakufanya ujihisi vizuri na kuelewa msimamo wa uhusiano wenu.
Kumtuliza mtu
Kama mna mabishano na mtu fulani, ni vyema kusema “nakupenda” ili kumjulisha kwamba ni kweli unampenda, japokuwa mnabishana.
Kumlinda mpenzi wako
Wakati watu wengine wanamshambulia mpenzi wako kwa sababu yoyote ile, huonekana kama kwamba watu wote wanapingana naye. Lakini ukimwambia “nakupenda” ni wazi unajionyesha kwamba utamlinda dhidi ya maneno yoyote ya kumshambulia na utawaonyesha wengine kwamba wewe na yeye mko pamoja.
Fahari
Wakati mmeo amepata mafanikio makubwa kama vile kupanda cheo kazini au kuimarisha afya yake, moja kwa moja utaona fahari kuwa mkewe. Hivyo, kumwambia “nakupenda” kutampa fahari.
Kujinufaisha

Unaweza kuwambia mtu “nakupenda” ukiwa na nia kwamba atakufanyia kitu fulani ambacho unakitaka. Hivyo, usione aibu kumwambia mtu yeyote neno hilo wakati wowote, iwapo utafaidika.

No comments:

Post a Comment

THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 1

Mtunzi: Hashim Aziz (Hashpower) 0719401968 “Ngo! Ngo! Ngo! Fungua!” “Nanii?” “Fungua!” “Jitambulishe kwanza, wewe nani?” “Nimese...