Wednesday, May 19, 2010

TO MY VALENTINE -17

“Brian why are you doing this to me, yaani unanikimbia kumbe unakuja kufurahi na huyu changudoa wako? Why Brian?” Nancy alioendelea kumlalamikia Brian ambaye alishindwa cha kujibu kwani kwa vyovyote ambavyo angemueleza Nancy asingemuelewa kutokana na mazingira aliyowakuta.

Kuingia kwa Nancy eneo lile ilikuwa na kama kuamsha kichaa kwa Ritta, kwani aliacha kila alichokuwa anakifanya na akawa anamsogelea Nancy kama nyati aliyejeruhiwa. Nancy naye alipania kumuonesha adui yake kuwa nayeye ni mtoto wa mjini. Alimsukumia Brian pembeni, wakavaana na Ritta na kuanza kurushiana makonde. Brian alijaribu kuwaamulia bila mafanikio, wakawa wanazidi kubiringishana chini kama wanamiereka. Alipoona mambo yanakuwa makubwa, Brian aliamua kuondoka bila kuaga, akaacha moto mkubwa unawaka.

“Nilikuwa nakutafuta sana hatimaye leo umejileta mwenyewe kwenye kumi na nane zangu, lazima nikuoneshe mimi ni nani?”
“Huniwezi kwa lolote malaya mkubwa wewe, kazi yako kuchukua waume za watu, sasa leo utajua kati yangu na wewe nani mwanamke zaidi.”
Ritta na Nancy walikuwa wakitupiana maneno machafu huku wakizidi kuburuzana chini. Rafiki zake Ritta walikuwa wakimsangilia shoga yao wakati akipigana wakiamini ushidi ulikuwa wao.

Puruushani zile ziliwapeleka mpaka kwenye keki aliyokuwa ameiandaa Ritta kwa ajili ya ulishana na Brian. Waliigonga na ikadondoka chini na kumeguka vipande vipande. Kwa jinsi Nancy alivyokuwa na hasira kali juu ya Ritta, alijikuta akiwa na nguvu ubwa kumzidi adui yake. Akawa anampa displini kiuhakika. Alipoona kama havimkolei, alijivutahadipale keki ilipodondokea. Akawahi kuokota kisu ilichokuwa kimeandaliwa maalum kwa ajili ya kuatia keki, akakishika wa mikono miwili na ukinyanyua juu.

Ritta alipoona adui yake ameshika kisu, akajua asipojiokoa huo ndiyomwisho wake.Akataka kumuwahi na kumpokonya, lakini akawa amechelewa. Nancy alimchoma Ritta begani kwa kutumia kile kisu, ghafla Ritta akaanza kupiga mayowe ya kuomba msaada huku damu zikimtiririka. Alipoona hivyo, Nancy aliwah kukimbilia nje alikomkuta yul edereva wa pikipiki aliyemleta akimsubiri. Akapanda juu na kumuamuru waondoke eneo hilo haraka.

Ritta aliendelea kupiga mayowe ya kuomba msaada, wale rafiki zake wakawa wanamsaidia kukitoa kile kisu na kuziba lile jeraha ili damu isizidi kumtoka zaidi mwenzao.

“Tumuwahishe hospitali, ushakuwa msala huu. Waliita Tax na kwa haraka wakamkimbiza Ritta Hospitali. Masihara ya kumchulia mwenzao kuwa yuko mahututi yaligeuka na kuwa kweli. Walipofika Hospitali waliambiwa kuwa hawawezi kutibiwa mpaka wapitie polisi na kupewa PF3. Kwa kuwa hali ya Ritta haikuwa nzuri ufuatia damu nyingi kumtoka, rafiki zake hawakuwa na ujanja zaidi ya kwenda naye kwanza kwenye kituo cha Polisi ambapo waliandikisha maelezo yao.

“Lazima aliyefanya kitendohiki akamatwe haraa iwezekanavyo.” Aliongea askari aliyeonekana kuwa mkubwa kuliko wenzie. Baada ya kuandikisha maelezo ambayo yaliwajumuisha Brian na Nancy, alipewa PF3 kisha safari ya kuelekea hospitali ikaanza upya. Polisi nao hawakutaka kupoteza muda, wakaingia mitaani kuanza kuwasaka watuhumiwa.

Baada ya kugundua kuwa amefanya kosa kubwa linaloweza kumtia mikononi mwa sheria, Nancy hautaka kulaza damu. Alirudi mpaka nyumbani kwao na kukusanya kila kilichokuwa chake. Bila hata kuaga akaondoka kuelekea jijni Arusha, kwani zilikuwa zimesalia wiki mbili tu kabla ya chuo kufungua. Alijua akiendelea kubakia nyumbani kwao, lazima mkono mrefu wa sheria ungemfikia na kumuweka korokoroni, kitu ambacho hakuwa tayari kuona kinatokea.

Upande wa pili, Brian hakuelewa nini kilichoendelea baada ya kuondoka na kuwaacha Nancy na Ritta wakipigana. Alijua kwa vyovyote wasingeweza kuumizana sana kwani mara nyingi ugomvi wa wanawake huishia kung’atana na kuparuana na makucha. Hakushtukia kuwa Nancy alikuwa amesababisha madhara makubwa , ambayo yagewaweka wote wawili hatiani. Baada ya kuukimbia ugomvi, alienda mpaka nyumbani kwake, lakini akili yake ikawa haijatulia kabisa, akaona ni vyema aende kwenye baa iliyokuwa jirani na pale kwao akapoteza mawazo kwa kunywa pombe.

Wakati Brian akiendelea kupiga moja moto moja baridi, alishtuka baada ya kuoa gari la polisi likipita mtaai kwao, na kwenda kusimama mbele ya nyumba aliyokuwa anaishi. Mapigo ya moyo yalianza kumwenda mbio, akahisi kuna hatari kubwa inayomfuata nyuma yake. Bila kupoteza muda, aliinuka haraka pale alipokuwa amekaa na kutokea mlango wa nyuma. ALipohakikisha hakua aliyemuona, alitimua mbio kwa uwezo wake wote kutokomea kusikojulikana

No comments:

Post a Comment

THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 1

Mtunzi: Hashim Aziz (Hashpower) 0719401968 “Ngo! Ngo! Ngo! Fungua!” “Nanii?” “Fungua!” “Jitambulishe kwanza, wewe nani?” “Nimese...