Wednesday, May 19, 2010

TO MY VALENTINE- 16

LICHA YA kujitahidi kumkwepa Ritta, Brian anajikuta kwa mara nyingine akinasa kwenye mtego ulioandaliwa na Ritta kwa kusaidiana na rafiki zake. Akiwa na mchumba wake Nancy, Brian anapigiwa simu na mtu anayejitambulisha kama rafiki yake Ritta kisha anamweleza kuwa mwenzake ana hali mbaya na yuko karibu kukata roho kwa ajili yake. Taarifa hiyo inamchanganya mno Brian, na anashindwa kuelewa nini cha kufanya. Japokuwa anamchukia Ritta kwa mambo anayomfanyia, lakini hayuko tayari kusikia yeye ndiyo chanzo cha matatizo ya Ritta. Anabaki njia panda.
Je atafanya nini? Nini kitatokea? Shuka nayo…

“Kwani vipi? Mbona sikuelewi? Huyo aliyekupigia simu ni nani?” Nancy alikuwa akiuliza maswali mfululizo ambayo yote Brian hakuyajibu. Alishangaa kuona Brian amebadilika ghafla baada ya kupokea simu ile. Nancy alijaribu kumtuliza Brian bila ya mafanikio, akatoka nje mbio mbio hata bila kuaga. Nancy alibaki ameduwaa sijue nini kilichomsibu mtarajiwa wake. Brian alipotoka tu, Nancy naye alianza kumfuata nyumanyuma ili kujua ni nini kilichokuwa kimempata.

“Haloo… eeh, umesema mgonjwa yuko wapi?” alikuwa akiuliza Brian kwa yule msichana aliyempa taarifa kuwa Ritta yuko mahututi.
“Bado tuko nyumbani kwake, tunajiandaa kumpeleka hospitali. Ukiwahi utatukuta nyumbani kwake.” Brian alivyosikia hivyo, alikodi Tax haraka na akamuamuru dereva amuwahishe mtaa anaoishi Ritta ili kwenda kuju nini kilikuwa kimemsibu. Huku nyuma, Nancy naye alikuwa akimfuatilia, alipoona amekodi Tax, yeye alikodi pikipik maarufu kama bodaboda na akamtaka dereva kuifuata ile Tax aliyokuwa amepada Brian.

Baada ya dakika kama ishirini kupita, tayari Brian alikuwa mbele ya nyumba aliyokuwa anaishi Ritta. Lengo lake kubwa ilikuwa ni kwenda kuhakikisha kama ile taarifa aliyopewa kwenye simu ni ya kweli au la. Hakutaka kuhusishwa na matatizo yoyote ambayo yangempata Ritta. Akilini mwake alihisi huenda ni kweli Ritta anaumwa sana hasa kutokana na ukweli kwamba aliaminishwa kuwa ana ujauzito wake, ingawa alikuwa ameingizwa mjini. Licha ya kuwa mwanzo alikuwa akikwepa kabisa kuitwa baba, baada ya ujauzito wa Nancy kuharibika alikuwa ni kama aliyechanganyikiwa.

AKiwa pale nje, alishusha pumzi ndefu na akawa anajiweka sawa kuingia ndani kumuona mgonjwa. Kitu kilichomshtua ni sauti kubwa ya muziki uliyokuwa inatoka kwenye chumba cha Ritta, akashindwa uelewa inawezekanaje chumba chenye mgonjwa mahututi kikawa na muziki mkubwa namna ile. Akaanza kuhisi amechezewa akili yake. Hata hivyo aliamua kuingia ndani kwenda kuhakikisha kwa macho yake mwenyewe. Aligonga mlango kwa nguvu, na rafiki yake Ritta akaenda kumfungulia.

Alipoingia ndani alishindwa kuamini macho yake, kwani Ritta aliyeambiwa yuko hoi taaban alikuwa akisakata muziki laini kwa madaha huku akionesha uwezo wake wa kuzugusha nyonga. Aligeuka huu na kule na akagundua kuwa alikuwa amedanganywa. Ritta alipomuona tu, alimkimbia na kusimama karibu naye, na kuanza kumsemesha kwa sauti ya kimahaba.

“Pole mpenzi, najua umeshtuka sana baada ya kusikia niko mahututi, nilijua nikikwambia ukweli hautakuja. Leo ni siku yangu ya kuzaliwa na nilitaka japo uje kutia baraka zako. Karibu ukae basi baba watoto,” aliogea Ritta huku akimshika mkono na kumuelekeza sehemu ya kukaa.
Kwa hasira alizokuwa nazo Brian baada ya kuona amegeuzwa bwege wa kuchezewa akili, alikataa kukaa na akamsukuma Ritta nyuma. Akawageukia rafiki zake waliokuwa wamenyamaza kimya wakiangalia kila kitu kilichokuwa kinaendelea.

“Nani kati yenu aliyenipigia simu? Sio kunitolea mimacho yenu, nauliza nai aliyenipigia simu kunipa taarifa za uongo?”

Hakuna aliyejibu zaidi ya wale rafiki zake Ritta kuanza kutazamana. Ritta aliingilia kati na kumwambia kuwa yeye ndiye aliyewatuma wampigie simu, kwa hiyo amalizane yeye mwenyewe. Kauli ile ya Ritta iliamsha hasira na chuki alizouwa nazo Brian, akajikuta mwili wote ukimtetemeka kwa hasira. Alimtazama Ritta kwa muda, lakn mwenyewe hakuonekana kujali, akaenda kuogeza suti ya redio na kuendelea kuyarudi mbele ya Brian. Rafiki zake waliangua vicheko vya kimbea vilivyommaliza nguvu, akawa mpole ghafla.

“Ukirudia ujinga wako ntakufunza adabu, usipende kuchezea akili yangu kama mtoto mdogo,” aliongea Brian kwa msisitizo, kisha akageuka na kuanza kutoka kuelekea nje. Kabla hata hajaufikia mlango, wote waliokuwa ndani walishtukia mlango ukisukumwa wa nguvu, waashangaa nancy akiingia mbiombio huku viatu vyake akiwa amevishika mkononi. Macho yake yakagongana na Brian aliyekuwa akijiandaa kuondoka.

No comments:

Post a Comment

THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 1

Mtunzi: Hashim Aziz (Hashpower) 0719401968 “Ngo! Ngo! Ngo! Fungua!” “Nanii?” “Fungua!” “Jitambulishe kwanza, wewe nani?” “Nimese...