Monday, May 10, 2010

PENZI LA CAREY LAMBADILISHA PINK


Licha ya mbwembwe na vurugu alizokuwa nazo katika siku za mwanzo za uhusiano wao, mwanamama Pink amejikuta akizidi kukolea kwenye penzi la Carey Hart, hali ambayo imemfanya abadili sana tabia yake kutoka kuwa mcharuko hadi kuwa mwanamke mwema. Awali uhusiano huo uliwahi kuvunjika kutokana na tabia ya ugomvi, matusi na kejeli alizokuwa nazo Pink kabla hajakolezwa kwenye malavidavi na Carey.
“Ni kweli siku za mwanzo nilikuwa simheshimu mpenzi wangu na nilikuwa nikifanya ninavyojisikia, lakini baada ya kutengana naye kwa muda, nimegundua kuwa ni mwanaume wa kipekee sana. Kwa sasa namheshimu sana na sitaki kumuudhi tena,” alikaririwa Pink wakati akihojiwa na mtandao mmoja mashuhuri nchini Marekani. Kwa sasa wawili hao wanafikiria kupata mtoto, ingawa wanasema kuwa ni mapema sana kulizungumzia jambo hilo.

No comments:

Post a Comment

THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 1

Mtunzi: Hashim Aziz (Hashpower) 0719401968 “Ngo! Ngo! Ngo! Fungua!” “Nanii?” “Fungua!” “Jitambulishe kwanza, wewe nani?” “Nimese...