Saturday, May 8, 2010

MAMA GEE, MERCY JOHNSON WAZICHAPA KAVUKAVU


Wasanii wawili wenye majina makubwa kunako ulimwengu wa filamu wa Nollywood, Patience Ozokwor a.k.a. Mama Gee na Mercy Johnson ambao wamekuwa na ugomvi wa muda mrefu, wamepigana hadharani na kuzua gumzo kubwa miongoni mwa mashabiki wao kutokana na kitendo hicho. Tukio hilo lililoelezwa kuwa aibu kubwa Nollywood, limetokea huko Ogwashi Ukwu, jimboni Delta, Nigeria wakati wakirekodi filamu.

Kwa mujibu wa mashuhuda, ugomvi huo ulianza baada ya Mercy kumtupia kauli mama chafu mama Gee wakati akiigiza, na kumwambia kuwa uwezo wake umeshuka sana na angeiharibu filamu wanayorekodi. Kauli hiyo ilijibiwa kwa hasira na Mama gee aliyemwambia Mercy yeye bado ni mtoto mdogo na hawezi kumfundisha lolote kunako game. Sekunde chache baadae wawili hao walivaana miilini, na kuanza kurushiana makonde, kanla ya ugomvi wao kuamuliwa na watu waliokuwa jirani.

No comments:

Post a Comment

THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 1

Mtunzi: Hashim Aziz (Hashpower) 0719401968 “Ngo! Ngo! Ngo! Fungua!” “Nanii?” “Fungua!” “Jitambulishe kwanza, wewe nani?” “Nimese...