Sunday, October 11, 2009

BEYONCE

BEYONCE AFANYA KWELI MOBO
Mwanadada Beyonce Knowles, mwimbaji mashuhuri wa RnB na Pop kutoka Marekani, ameng’ara kwenye tuzo za (Music of Black Origin) MOBO na kufanikiwa kunyakua tuzo mbili kwa mpigo. Sherehe za utoaji tuzo hizo zilifanyika juzi kat (Tarehe 30 mwezi Septemba) katika ukumbi wa SECC, huko Glasgow Scotland, na ziliwashirikisha wasanii weusi kutoka pande zote za dunia.

MOBO ni tuzo zinazotolewa kwa wasanii weusi pekee waliofanya vizuri katia medani ya muziki wa kimataifa na hufanyika kila mwaka. Kwa mwaka huu Beyonce ameondoka na tuzo mbili kwa mpigo, Msanii Bora wa Kimataifa (Best International Act)
na video bora ya wimbo wa “Single Ladies, (Put a Ring On It)” Wasanii wengine waliojinyakulia tuzo hizo ni pamoja na:
Wasanii wanaochipukia – JLS, wimbo bora- JLS - Beat Again, Albamu bora- N-Dubz, Dj bora- Trevor Nelson, Mwanahiphop bora – Chipmunk, Msanii bora wa R&B - Keri Hilson, Mwanamuziki bora wa kimataifa- Beyonce, Video bora- Beyonce - Single Ladies, Msanii bora wa Reggae - Sean Paul, msanii bora wa Jazz - Yolanda Brown, Msanii bora wa Gospel - Vic Tizzle Na msanii bora kutoka Afrika - Nneka. Pia Mobo ilitoa tuzo ya heshima kwa marehemu Michael Jackson ambaye aliwakilishwa na ndugu zake La Toya na Jermaine Jackson.
Beyonce ameelezea kupata tuzo hizo kama mafanikio makubwa kwake na ameahidi kuendelea kukaza buti. Kwa sasa mwanadada huyo anatamba na albamu yake ya “A im Sasha…Fierce”

No comments:

Post a Comment

THE DARKEST HOURS (SAA ZA GIZA TOTORO)- 1

Mtunzi: Hashim Aziz (Hashpower) 0719401968 “Ngo! Ngo! Ngo! Fungua!” “Nanii?” “Fungua!” “Jitambulishe kwanza, wewe nani?” “Nimese...